Ads (728x90)


Na,Thompson Mpanji,Iringa.

WITO umetolewa kwa vyombo vya habari nchini kukitumia kipindi kilichobaki  hadi siku ya sensa kuongeza kasi ya utangazaji wa taarifa ya sensa kwa kupeleka ujumbe sahihi kwa wananchi ikiwemo na kusisitiza kauli mbiu ya taifa kuwa, "Sensa kwa maendeleo,jiandae kuhesabiwa".

Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Dkt.Christina Ishengoma ametoa wito huo wakati wa ufunguzi wa semina ya sensa kwa waandishi wa habari wa mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini na mikoa ya Lindi na Mtwara yaliyomalizika jana(Agosti,12) katika ukumbi wa Chuo kikuu cha Ruaha(RUCO).

Dkt.Ishengoma alisema licha ya kauli mbiu wanahabari  wanashauriwa kuwaeleza wananchi vidokezo muhimu kuhusu umuhimu wa zoezi zima la sensa ili waweze kujiandaa vema.

Alitaja vidokezo muhimu ni pamoja na siku ya kuanza kufanyika zoezi la sena agosti,26,2012 ambapo watakaohesabiwa ni waatanzania watakaokuwa nchni Tanzania usiku wa jumamosi agosti,25 kuamkia agosti,26,2012.

Alifafanua kuwa watu watakaohesabiwa  katika kaya ni wale watakaokuwa wamelala katika kaya usiku  wa kuamkia siku ya sensa pamoja na wanakaya wanaofanyakazi za usiku  ambao kwa usiku huo hawakulala kwenye kaya wakiwemo watumishi wa sekta ya afya,ulinzi na usalama sanjari na sekta ya habari.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa msisitizo kwa wakuu wa kaya kuweka kumbukumbu sahihi za watu wake wote zikiwemo za umri,kiwango cha elimu,ajira anayofanya,mahali anaposhinda mwanakaya wakati wa mchana na kwa wanawake hali zo za uzazi.





Post a Comment