Ads (728x90)



MJI wa Mombasa uliopo Pwani ya nchi ya Kenya umekumbwa na machafuko na hali ya taharuki kwa waumini wa Kiislamu kufuatia kuuawa kwa Sheikh Aboud Rogo ambaye awali alidaiwa kutuhumiwa kuhusishwa na kikundi cha kigaidi cha El Shabab.
Kifo cha Sheikh Rogo ambaye ameuawa mapema siku ya Jumatatu kimesababisha machafuko katika mji huo huku baadhi ya  watu wakielezwa kuingia katika vurugu na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa.
Sheikh Rogo aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa  ndani ya gari lake ambapo siku kadhaa aliwahi kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za ugaidi, aliachiwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi wa uhusika wake juu ya vitendo vya ugaidi, mkewe wa mtuhumiwa huyo wa Ugaidi anaelezwa kujeruhiwa katika sakata hilo.
Mashuhuda wanaelezea tukio hilo kuwa Sheikh Rogo alipigwa risasi akiwa katika mwendo kasi ndani ya gari lake.
Mwezi uliopitaa mahakama ya mjini Nairobi ilimuamuru mkuu wa kituo cha Polisi cha Kamukunji kumchunguza Sheikh Rogo na Sherif Abdullahi ambapo askari polisi waliwakamata wakiwa njiani kuelekea mjini Nairobi.
Hayati Rogo na Sherrif walikuwa wakisafiri kutokea mjini Mombasa kuelekea Nairobi ili kuhudhuria mahakamani ambako walifunguliwa kesi juu ya tuhuma za vitendo vya ugaidi na mauaji.
Hayati Rogo amezikwa katika makaburi ya Kikowani kwa mila na desturi zote za dini ya kiislamu.(chanzo thecitizen Kenya)

Post a Comment