Na, Rashid
Mkwinda, Mbeya
MTU mmoja
amekufa papo hapo na wengine 11 kujeruhiwa vibaya kwenye ajali iliyohusisha
magari matatu katika eneo la Nzovwe jijini Mbeya baadaa ya Lori aina ya Leyland
DAF kufeli breki na kuzigonga kwa nyuma Hiace mbili zilizokuwa zikifanya safari
zake kati ya Mwanjelwa na TAZARA.
Mashuhuda wa
ajali hiyo walidai kuwa lori hilo lenye namba za usajili T 721 BVD na Trela
lenye namba T 668 BGZ lililokuwa likielekea barabara Zambia liliigonga Hiace yenye
namba T 945 AFG ambayo nayo iliigonga
Hiace nyingine yenye namba za usajili T 150 AJL ambazo zote zilikuwa zimesimama
kwa muda eneo la Kalobe zikishusha abiria.
Mmoja wa
mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina la Maimuna Abdallah alisema kuwa
aliliona Lori hilo lenye trela likishuka kwa mwendo wa kasi eneo la Nzovwe na
baadaye likaigonga Hiace kwa nyuma ambayo ilipinduka upande wa kushoto kabla
haijaigonga Hiace nyingine ambayo nayo ilipinduka.
Gazeti hili
lilishuhudia majeruhi walioumia vinaya wakipatiwa huduma katika hospitali ya
rufaa Mbeya na kulazwa ambapo watatu kati ya majeruhi hao wamelazwa katika wodi
ya wagonjwa mahututi.
‘’Tumepokea
majeruhi 11 wote hali zao ni mbaya wamelazwa katik wodi namba 1 na namba 2
watatu hali zao ni mbaya zaidi wako chini ya uangalizi maalumu,’’alisema
Muuguzi mkuu wa Hospitali ya rufaa Mbeya Dkt. Thomas Isdory.
Aidha Dkt.
Isdory alisema kuwa wamepokea mwili wa mtu mmoja mwanaume ambaye alikutwa na
tiketi yenye jina la Joshua anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25-30.
Aliwataja
majeruhi waliolazwa hospitalini hapo kuwa ni Said Omar, William Claud,Jesse
Joseph, Eliah, Ambakisye, Josia Chonga, Godi Sanga, Nasra Nyagawa, Jane Mligo
na wawili ambao bado majina yao hayajatambuliwa.
|
Post a Comment