MKUU wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewapa somo waislamu ambo walikuwa na desturi ya kupiga majungu, badala yake wajikite katika kazi za maendeleo ambazo zitaongeza vipato vyao na kuwainua kiuchumi.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha Mfuko wa Maendeleo kwa Waislamu wa Mkoa wa Mbeya MRIDEF, Bw. Kandoro alisema ni fursa kwa waislamu kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao kwa ujasiriamali na kuongeza vipato vyao. Alisema kuwa kitendo cha wazazi wengi kuona elimu ya dunia ni kitu cha mchezo kimesababisha kudorora kwa maendeleo ya waislamu mmoja mmoja hivyo ni vyema waislamu wakathamini uwepo wao duniani kwa kufanya yale ambayo Mwenezi Mungu ameagiza.Kwa upande wake Katibu wa Mfuko wa Maendeleo MRIDEF Shekhe Abbas Mshauri alisema kuwa dhamira ya kuanzisha mfuko huo umelenga kusaidia maendeleo ya waislamu kielimu na kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwekeza vitega uchumi vinavyokwenda mnasaba na maadili ya dini ya Kiislamu. |
|
|
|
Post a Comment