Ads (728x90)

MKURUGENZI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA NHC NEHEMIA MCHECHU AKIPANDA MTI WA KUMBUKUMBU WAKATI WA JUBILE YA MIAKA 50 YA SHULE YA SEKONDARI YA MBEYA DAY AMBAYO NDIYO ALIYOSOMA NA KUMALIZA MIAKA YA 90

MKUU WA WILAYA YA MBEYA DKT. NOUMAN SIGALLA AKIPANDA MTI WA KUMBUKUMBU WAKATI WA SHEREHE YA KUADHIMISHA JUBILEI YA MIAKA 50 YA SHULE YA SEKONDARI YA MBEYA DAY LEO ASUBUHI

MKUU WA WILAYA YA MBEYA DKT. NOUMAN SIGALLA NA MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI WAKIJADILIANA JAMBO NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA NHC NEHEMIA MCHECHU WAKATI WA MAADHIMISHO YA JUBILEI YA MIAKA 50 YA SHULE HIYO LEO ASUBUHI, MCHECHU NA SUGU WAMESOMA SHULE HIYO MIAKA YA 90
JUBILEI YA MIAKA 50 YA SHULE YA SEKONDARI YA MBEYA MAARUFU KWA JINA LA MBEYA DAY LEO ILIMKUTANISHA MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI 'SUGU' NA BAADHI YA WALIMU WAKE WA ZAMANI NA KUONESHA HISIA ZAKE KWAMBA SHULE HIYO NDIYO ILIMPATIA UMAARUFU ALIONAO KWA SASA.

SUGU AMBAYE PIA NI MUASISI WA MUZIKI WA KUFOKAFOKA NCHINI MAARUFU KWA JINA LA HIP HOP NAKUMBUKA NAMNA AMBAVYO ALIVYOKUWA AKISHIRIKI MASOMO NA ZAIDI YA HAPO NAMNA AMBAVYO YEYE BINAFSI NDIKO AMBAKO KIPAJI CHAKE CHA MUZIKI WA HIP HOP KILIPOANZIA

''WADOGO ZANGU NA WENGINE NI WANANGU HAPA SHULENI NATHAMINI MCHANGO WA SHULE HII KATIKA MAFANIKIO YANGU YA KIMAISHA MIMI NIMESOMA KATIKA SHULE HII, NITASHIRIKIANA NANYI KWA HALI NA MALI KUHAKIKISHA SHULE HII INASONGA MBELE''

SUGU AMBAYE ALICANGIA KIASI CHA SH. MILIONI MOJA KATIKA HARAMBEE YA CHAPCHAP ILIYOANDALIWA KWA AJILI YA KUCHANGIA UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU NA BWENI LA WASICHANA ALISEMA KUWA ANAAMINI WANAFUNZI WAKIENDELEZWA KATIKA VIPAJI VYAO WATAFIKIA MATARAJIO YAO YA KIMAISHA.

KWA UPANDE WAKE MGENI RASMI WA JUBILEI HIYO AMBAYE PIA ALIWAHI KUSOMA SHULE HIYO MIAKA YA MWANZONI MWA TISINI AKIWA PAMOJA NA SUGU AMBAYE NI MKURUGENZI WA SHIRIKA LA NYUMBA TANZANIA, NEHEMIA MCHECHU ALISEMA KUWA  ANA IMANI KABISA KUWA VIPAJI WALIVYONAVYO WANAFUNZI VIKIENDELEZWA NDIVYO AMBAVYO VITASAIDIA KUWAKOMBOA KATIKA MAISHA YAO YA USONI.

MCHECHU ALIVUTA ZAIDI HISIA ZA WANAFUNZI HAO ALIPOWAKUMBUSHA BWENI ALILOKUWA AKILALA ENZI HIZO PAMOJA NA SUGU NA KUSEMA KUWA KAMWE WANAFUNZI WASIKUBALI KUITWA WALALAHOI KWANI WANAZO FURSA ZA KUWAFANYA WASIWE WALALAHOI



Post a Comment