Nyumba ya Mkuchika inawaka moto-Newala
Taarifa za
redio mbao sasa ni kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu
mkubwa huko ambapo naambiwa wamevamia gereza wakafungulia wafungwa na
kisha kupiga moto gereza. Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni
wanarusha mabomu yao tokea huko walikojificha maana nje hakutamaniki. Na
wameshateketeza nyumba ya mama Anna Abdallah.
Update:
Kikao cha
dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa kuwashirikisha
maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es Salaam kuongezea
nguvu.
Maaskari na makachero wawasili Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.
Hosteli
ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi maeneo ya Kiyangu B Mtwara yakoswa
koswa kuchomwa moto kwa kile kinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa
Ghasia mpaka sasa wanafunzi hawana mahala pa kukaa. Kituo kidogo cha
Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara nacho chakoswa na moto. Ofisi ya Afisa
Mtendaji Nkanaledi mkoani Mtwara nayo yavunjwa.
Wananchi
wamechoma moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za
waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani
(Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani.
Wakiwa
katika mahakama ya mwanzo, Polisi walizingirwa na vijana waliokuwa
wamebeba mawe na kufunga barabara zote za kuingia na kutoka Kituo Kikuu
cha Mabasi na eneo la Soko Kuu, licha ya kufyatua hewani mabomu ya
machozi.
Baadhi ya barabara za zimezibwa kwa kuchomwa matairi ya gari, na kuongeza hofu kwa wananchi.
Hali
imeshakuwa mbaya masasi taarifa zilizotufikia punde wamechoma eneo
linaloitwa loliondo, ofisi za elimu na ofisi ya trafiki, inasemekana
jamaa wameshavamia ofisi za halmashauri wengine wako njiani nyumbani kwa
mama Ana Abdala, hapa Mtwara mjini maduka yote eneo la soko kuu na
stendi yamefungwa hakuna huduma, huko Newala , leo kuna mkutano mkubwa
mchana huu wa kumkataa George Mkuchika.
Vurugu
zahamia wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Nyumba ya Mbunge wa Masasi nayo
yateketezwa kwa Moto hivi sasa...Madereva Bodaboda waandamana ...Vurugu
zashamiri Mabomu Kibao..Hali ni tete
Updates
- Kikao
cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa
kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es
Salaam kuongezea nguvu.
- Maaskari
na makachero wamewasili Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea
nguvu.Maaskari na makachero wawasili Mtwara leo asubuhi na helkopta
kuongezea nguvu.
- Hosteli
ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi maeneo ya Kiyangu B Mtwara yakoswa
koswa kuchomwa moto kwa kile kinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa
Ghasia mpaka sasa wanafunzi hawana mahala pa kukaa.
- Kituo
kidogo cha Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara nacho chakoswa na moto.
Ofisi ya Afisa Mtendaji Nkanaledi mkoani Mtwara nayo yavunjwa.
- Wananchi
wamechoma moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za
waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani
(Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani.
- Wakiwa
katika mahakama ya mwanzo, Polisi walizingirwa na vijana waliokuwa
wamebeba mawe na kufunga barabara zote za kuingia na kutoka Kituo Kikuu
cha Mabasi na eneo la Soko Kuu, licha ya kufyatua hewani mabomu ya
machozi.
- Baadhi ya barabara za zimezibwa kwa kuchomwa matairi ya gari, na kuongeza hofu kwa wananchi.
- Hali
imeshakuwa mbaya Masasi taarifa zilizotufikia punde wamechoma eneo
linaloitwa loliondo, ofisi za elimu na ofisi ya trafiki, inasemekana
jamaa wameshavamia ofisi za halmashauri wengine wako njiani nyumbani kwa
mama Ana Abdala, hapa Mtwara mjini maduka yote eneo la soko kuu na
stendi yamefungwa hakuna huduma, huko Newala , leo kuna mkutano mkubwa
mchana huu wa kumkataa George Mkuchika.
- Vurugu
zahamia wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Nyumba ya Mbunge wa Masasi nayo
yateketezwa kwa Moto hivi sasa...Madereva Bodaboda waandamana ...Vurugu
zashamiri Mabomu Kibao..Hali ni tete
Askari auawa Na
taarifa zaidi kutoka Masasi zinaeleza kuwa askari wa upelelezi Masasi
aliyejichanganya katika vurugu wananchi walimshitukia akiwapiga picha,
akashambuliwa na kuuliwa. Askari huyo inaelezwa amekutwa na bastola
mbili. Taarifa zaidi baada ya kuthibitishwa tutawaletea.(KWA HISANI YA BLOG YA MTWARA KUMEKUCHA NA JUMA MTANDA) |
Post a Comment