TAARIFA YA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE”
TAREHE 14.01.2013.
WILAYA
YA MOMBA – MAUAJI
MNAMO TAREHE 13.01.2013 MAJIRA YA SAA
12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KALUNGU KIJIJI CHA IVUNA TARAFA YA KAMSAMBA
WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. WATU WAWILI AMBAO NI 1.ERNEST S/O TWINI MOLELA NA MIZINARA
D/O MILILO @ MATELA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IVUNA WALIUAWA KWA KUPIGWA NA
WATU WASIOFAHAMIKA KISHA KUWAZIKA KATIKA KABURI MOJA . CHANZO NI TUHUMA ZA
KISHIRIKINA BAADA YA MAREHEMU HAO KUTUHUMIWA KUWA NI WACHAWI KWA KUMLOGA
MAREHEMU NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA
ALIYEFARIKI DUNIA TAREHE 12.01.2013 MAJIRA YA SA 16:00HRS BAADA YA KUUGUA MUDA MREFU.
TUKIO HILO LILITOKEA WAKATI WA MAZISHI YA MAREHEMU NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA AMBAPO KUNDI LA WATU WASIOPUNGUA KUMI
WALIPANDISHA HASIRA NA KUWATUHUMU MAREHEMU HAO KUHUSIKA NA KIFO CHA NDUGU YAO NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA HIVYO KUANZA
KUWASHAMBULIA KWA KUTUMIA NGUMI, FIMBO NA MAWE KISHA KUWATUMBUKIZA KATIKA
KABURI ALILOKUWA AKIZIKWA MAREHEMU NONGWA
S/O HUSSEIN MOLELA WAKIWA HAI NA KUWAZIKA WOTE WATATU KATIKA KABURI HILO
MOJA. BAADA YA HAPO WATU HAO WALIKWENDA NYUMBANI KWA ERNEST S/O TWINI MOLELA NA KUICHOMA MOTO NYUMBA YAKE. KUFUATIA
TUKIO HILO WATUHUMIWA WAWILI WALIOKUWA VINARA WA TUKIO HILO WAMEKAMATWA AMBAO
NI 1. VENA S/O ERNEST MOLELA [MTOTO
WA MAREHEMU ERNEST S/O TWINI MOLELA], MIAKA 26, MUWANDA, MKULIMA NA 2. EMANUEL S/O CHRISTOPHA, MIAKA 16,
MUWANDA MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IVUNA. MAREHEMU WOTE WATATU NI NDUGU WA UKOO MMOJA. TARATIBU
ZA KUFUKUA KABURI ILI MIILI YA MAREHEMU IFANYIWE UCHUNGUZI ZINAFANYWA. AIDHA TARATIBU
ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE MAHAKAMANI.KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAHESHIMU NA KUTII SHERIA PASIPO KUSHURUTISHWA. PIA
ANAIASA JAMII KUACHANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KWA
JAMII IKIWA NI PAMOJA NA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO. AIDHA ANATOA RAI KWA
JAMII/KIKUNDI CHA WATU WENYE KERO/MALALAMIKO,USHAURI ,UJUMBE MAALUM KUTAFUTA
NJIA ILIYO HALALI KUFIKISHA KERO,MALALAMIKO,USHAURI ,UJUMBE WAO KWA NJIA YA
MAZUNGUMZO BADALA YA KUTUMIA VURUGU/FUJO NA KUSABABISHA MAUAJI.
Post a Comment