BIBI SOMOE ISSA AJUZA ALIYETISHIA GESI KUGEUKA MAJI |
MHARIRI WA BLOG YA KUSINI AKIANGALIA MABAKI YA GARI LILILOCHOMWA MOTO NA WANANCHI KIJIJI CHA MSIMBATI |
BAADHI YA WANANCHI WA MSIMBATI WAKIANGALIA MABAKI YA GARI LILILOCHOMWA MOTO |
AISHA HAMISI MTOTO WA AJUZA ALIYETISHIA GESI KUGEUKA MAJI |
Na, Waandishi wetu Mtwara
SAKATA la gesi ya Mtwara
limechukua sura mpya bada ya Ajuza mwenye umri wa miaka 90 kutishia kuwa iwapo
gesi hiyo itasafirishwa kuelekea Jijini Dar es salaam itageuka maji.
Ajuza huyo mkazi wa Msimbati
Mtwara inakotokea gesi hiyo Somoe Issa(90) ambaye ametambulishwa kuwa ni mkuu
wa kaya ya Msimbati inadaiwa kuwa mara baada ya kutamka maneno hayo alianza
kufuatiliwa na viongozi wa serikali.
Taarifa zaidi zinadai kuwa bi
mkubwa huyo aliandaliwa safari ya kuondoka kijijini hapo kwa gari maalumu hali
ambayo iliibua hofu kwa wanakijiji ya kwamba huenda bibi huyo angetoweka katika mazingira ya
kutatanisha.
Kwa mujibu wa taarifa hizo ni
kwamba kijiji hicho cha Msimbati ndicho a,mbacho miradi ya uvunaji wa gesi hiyo
asilia ilipo na kwamba mtu mmoja anayedaiwa kuwa ana asili ya kijiji hicho
aliwasili kijijini hapo akiwa na gari ndogo aina ya Mark II kwa nia ya kwenda
nyumbani kwa shangazi yake .
Inaelezwa kuwa majira ya saa
mbili usiku alikwenda nyumbani kwa bibi Mtiti akiwa na gari hiyo kwa maelezo
kuwa alikuwa akienda kwa shangazi yake aliyetambulika kwa jina la Fatuma Said
Tom.
Hata hivyo imedaiwa kuwa
wakazi wa kijiji hicho wameweka ulinzi kwa bibi huyo kwa madai kuwa kufuatia
taarifa alizotoa juu ya tishio la gesi hiyo kugeuka maji kwamba amekuwa
akisakwa kwa udi na uvumba kwa nia ya kupotezwa katika mazingira ya
kutatanisha.
Mkazi wa kijiji hicho
aliyejitambulisha kwa jina la Juma Ayoub alisema kuwa wakazi wa maeneo hayo
walilifuatilia gari hilo kwa karibu mara walipoliona nyakati za usiku.Naye Asha
Hamisi alisema kuwa yapata majira ya saa mbili usiku walikuja watu wawili ambao
walihitaji kuongea na Bibi huyo wakidai kuwa wanataka kwenda naye Mtwara.
Alisema kuwa watu hao walidai
kuwa wametumwa na Rais Kikwete na Hawa Ghasia wazungumze na bibi huyo kuhusu
mambo ya gesi na kwamba iwapo bibi huyo yupo tayari watamfuata jumanne ijayo
ili waondoke naye.
Hata hivyo anasema kuwa wakiwa
katika majadiliano hayo ghafla alipochungulia nje aliona umati wa watu
wamekusanyika.
Naye Manzi Mohamed Faki
ambaye ni motto wa tano wa bibi huyo anasimulia kuwa walimfuata jamaa huyo
kwamba aondoke eneo hilo na afute wazo alilojia na kwamba walimsihi kwa muda
mrefu aondoke lakini hakuwasikiliza na kwamba kadri muda ulivyozidi kusonga
ndivyo ambavyo watu waliendelea kujaa eneo hilo na kuanza kumrushia mawe ambapo
alikimbia na kutelekeza gari lake ambalo na hatimaye liliteketezwa kwa moto.
Kwa upande wake shangazi wa
kijana huyo ambaye gari lake liliteketezwa kwa moto Fatuma Tom alisema kuwa
alimpokea mwanaye ambaye alimuomba amsindikize kwa bibi huyo ambapo alisema
kuwa yeye ametumwa na wakubwa wake wa kazi amchukue bibi huyo aende naye Dar es
salaam.
‘’Huyu ni mwanangu mtoto wa kaka yangu anaishi
Dar es salaam anafanya kazi usalama wa Taifa’’ alisema Bibi Tom.
Mwenyekiti wa kijiji hicho
Salum Tostao alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini alisema kuwa ofisi
yake haina taarifa ya kumpokea mgeni wa kiserikali na kwamba gari lililoteketea
kwa moto ni mali ya Mussa Babu lenye namba za usajili T 609 BXG.Kamanda wa
polisi mkoa wa Mtwara Maria Nzuki amedai kuwa hana taarifa za tukio hilo kwa
madai kuwa hakuna mtu aliyelalamika kuchomewa moto gari lake.(taarifa
hizi ni kwa hisani ya Hassan Samli wa Mtwara na blogu ya kusini zilizotolewa
kwenye mtandao wa jamii forums)
Post a Comment