NAIBU Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Bw. Kassim Majaliwa juzi alijionea vioja katika shule ya Msingi Nkala iliyopo wilayani Momba mkoani Mbeya baada ya kukutana na wanafunzi wa darasa la saba ambao hawajui kusoma wala kuandika.
Majaliwa alikutana na kioja hicho alipotembelea shule hiyo na kuingia moja kwa moja darasani alikowakuta wanafunzi wamekaa katika madawati huku wakiwa na vitabu vyao wakionesha dalili za kujisomea.
Baada ya kuona umakini wa wanafunzi hao Majaliwa alihamasika kuwaliza maswali mepesi mepesi wanafunzi hao ikiwemo hesabu za 1 x 2 na 2 x 5, na 2-2 ambapo wanafunzi hao walizichangamkia kujibu maswali hayo bila wasiwasi wowote.
Mara baada ya kuona kwamba wanafunzi wale huenda ni waelewa Naibu waziri alichukua moja ya vitabu vilivyopo darasani humo, Kitabu cha somo la Uraia na kumchagua mmoja wa wanafunzi ili asome sentensi iliyopo katika kitabu hicho ndipo, patashika ilipoanza.
Mwanafunzi wa kwanza aliposhindwa kusoma alimchagua mwanafunzi mwingine asome naye alishindwa na kumchagua mwingine ambaye pia alishindwa, kisha mwalimu mkuu wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Godfrey Mwanguo alipojitetea na kusema kuwa walimu wanapata wakati mgumu kuwafundisha wanafunzi hao kutokana na tatizo la lugha kwani wanafunzi hao wanapenda zaidi kutumia lugha yao ya asili ya Kinyamwanga.
Hata hivyo utetezi huo haukumwingia vyema Naibu Waziri na kusema kuwa kama ni kweli wanafunzi hao wameathiriwa na lugha yao ya asili wasingeweza kuelewana katika mazungumzo yao ambapo aliwauliza kwa lugha ya kiswahili na wao walijibu bila kubabaika ikiwa na maana kwamba sio kwamba hawaelewi kiswahili.
‘’Nyie
mnasoma darasa la ngapi?’’aliuliza Bw. Majaliwa ambapo wote kwa pamoja
walijitambulisha kuwa wanasoma darasa la saba.
|
Post a Comment