WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, BERNARD MEMBE |
BAADHI YA WAHITIMU YA WANAZUONI WAHITIMU WA VYUO VYA TEKU NA MZUMBE WANAJUMUIYA WA KANISA KATOLIKI WAKIFUATILIA KWA MAKINI HOTUBA ZA VIONGOZI |
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA (NEC) SAMBWEE SHITAMBALA AKITETA JAMBO NA ASKOFU WA KANISA KATOLIKI JIMBO LA MBEYA EVARIST CHENGULA |
STORI NA RASHID MKWINDA
WAZIRI wa Mambo
ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Bernard Membe ametoa angalizo
kwa watu wanaohitaji msaada wa fedha kutoka kwa baadhi ya wanasiasa kuwa na
tahadhari na fedha hizo kwa kuwa baadhi yake ni fedha ambazo zimetokana na
ufisadi.
Kauli hiyo
ya Bw. Membe ilitolewa kwa niaba yake na Mjumbe wa halmashauri kuu CCM Taifa
Bw. Sambwee Shitambala jijini Mbeya mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa chuo
kikuu cha TEKU huku kukiwa na wimbi la baadhi ya wanasiasa kutajwa kuwania
kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2015.
Baadhi ya
wanasiasa wanaotajwa kuwania urais kupitia CCM ni pamoja na Mbunge wa
Monduli,Bw. Edward Lowassa,Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Samwel
Sitta na Bw. Membe.
Akizungumza wakati
wa mahafali ya Jumuiya wanafunzi wa katoliki elimu ya Juu MUCCASA jijini Mbeya Bw.
Shitambala alisema kuwa yeye ametumwa kumwakilisha Bw. Membe katika mahafali
hiyo ambapo alisema kuwa amewaagiza kuwa na tahadhari na fedha za baadhi ya
wanasiasa wanaochangia makanisa.
Alisema kuwa
kuna haja ya kuwa na vyanzo vya fedha halali ambazo zitatumika kihalali badala
ya kuwa na fedha chafu ambazo zinatumika kwa kisingizio cha kutoa misaada
katika taasisi mbalimbali za kijamii.
‘’Fedha
chafu zisiingizwe kwenye mambo ya dini, tuwaangalie hawa wanasiasa wanaokuja na
kumwaga fedha kwa kisingizio cha kusaidia jamii,’’alisema.
Awalin
akizungumza na wanazuoni hao Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya Evarist
Chengula aliwaasa vijana hao kutojiingiza katika migongano na migomo inayoweza
kusababisha migogoro ya kijamii na kuhatarisha amani na utulivu wa nchi yetu.
Askofu
Chengula alisema kuwa elimu waliyoipata itumike kwa maslahi ya Taifa ikiwa ni
pamoja na kudumisha amani na utulivu uliopo badala ya kujiingiza katika makundi
ambayo yameonesha nia ya kuliingiza Taifa kwenye vurugu.
‘’Taifa
linahitaji mchango wenu katika kudumisha amani na utulivu, nyinyi ni kundi
kubwa le nye nguvu, mkitumika vizuri amani itapatikana, mkitumika vibaya,
mtaliingiza Taifa letu kwenye majanga,’’alisema Askofu Chengula.
Post a Comment