BAADHI YA WANAHABARI NA WANACHAMA WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA WAKISIKILIZA KWA MAKINI TAARIFA KUTOKA KWA MAOFISA WA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU |
MRATIBU WA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU ONESMO OLENGURUMWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KWENYE OFISI YA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA |
BAADHI YA WANAHABARI WANACHAMA WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MAOFISA WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU |
MTANDAO WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA UMETOA SOMO
KWA WANAHABARI MKOANI MBEYA KUJITAHIDI KUKABILIANA NA MAZINGIRA HATARISHI YA UITENDAJI KAZI KWA KUJIHAMI KABLA YA
KUKUTWA NA MATATIZO AU MAAFA WAWAPO KAZINI.
AKIZUNGUMZA
KATIKA KIKAO MAALUMU KATI YA WANAHABARI WA MKOA WA MBEYA NA WATETEZI HAO WA
HAKI ZA BINADAMU KWENYE OFISI YA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA,
MRATIBU WA MTANDAO BW. ONESMO OLE NGURUMWA ALISEMA KUWA WANAHABARI WANATAKIWA
KUWA MAKINI KATIKA UTENDAJI WAO ILI KUEPUKA KUPATA MADHARA.
ALISEMA KUWA
ASILIMIA KUBWA YA WAANDISHI WA HABARI WA TANZANIA WANAFANYA KAZI KATIKA
MAZINGIRA YANAYOHATARISHA MAISHA YAO KUTOKANA NA MFUMO ULIOPO KATIKA JAMII
INAYOWAZUNGUKA NA HIVYO KUSHINDWA KUTEKELEZA WAJIBU WAO IPASAVYO.
BW. OLENGURUMWA
ALISEMA KUWA MFUMO WA WAANDISHI WOTE NCHINI UNAFANANA HIVYO NI WAJIBU WAANDISHI
WENYEWE KUJIHADHARI NA KUWA MAKINI KATIKA UTEKELEZAJI WAO WA KAZI KWA KILA
SIKU.
ALISEMA
WANAHABARI NI SEHEMU YA KIUNGO MUHIMU ZA KUTOA TAARIFA ZA MIGOGORO MBALIMBALI
YA KIJAMII KAMA VILE MAENEO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI, HAKI ZA WATOTO,
UNYANYASAJI WA KIJINSIA PAMOJA NA UFUATILIAJI WA TAARIFA ZA KUTOWAJIBIKA KWA
WATENDAJI KATIKA SEKTA ZA IDARA ZA SERIKALI AMBAZO BAADHI YAKE ZINAGUSWA NA
MATATIZO YA RUSHWA.
ALISEMA
KUTOKANA NA HALI HIYO WANAHABARI WANAPASWA KUJUA KUWA KUNA BAADHI YA WATU
WATAGUSWA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE NA HIVYO KUJENGA UADUI MIONGONI MWA
MAENEO HAYO AMBAYO YANAHITAJI KUPATIWA UFUMBUZI KWA TAARIFA ZA WANAHABARI.
KWA UPANDE
WAKE OFISA HABARI WA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU BW. ELIAS MHEGERA
ALISEMA KUWA WAKO KATIKA URATIBU WA KUIBUA MATATIZO YANAYOWAKUMBA WANAHABARI
KATIKA MAENEO YAO YA KAZI NCHINI AMBAPO MTANDAO UTAANDAA MAFUNZO KWA WANAHABARI
ILI KUONGEZA WELEDI NA UTENDAJI KAZI KWA
WANAHABARI NCHINI.
BW. MHEGERA
ALISEMA KUWA MAZINGIRA YA WANAHABARI KOTE NCHINI YANASHABIHIANA AMBAPO BAADHI
YAO WAMEJIKUTA WAKIWA MAADUI KATIKA JAMII WANAYOISHI KUTOKANA NA UTENDAJI WAO
NA HIVYO KUJIKUTA WAKO KATIKA HATARI PAMOJA NA KWAMBA WAO NI SEHEMU YA MSAADA
KWA JAMII HIYO.
NAO BAADHI YA WANAHABARI WA MKOA WA MBEYA WALISEMA KUWA WAMEKUWA WAKIKUTANA NA CHANGAMOTO NYINGI KATIKA UTENDAJI WAO IKIWEMO KUPIGWA NA KUVUNJIWA VIFAA VYAO VYA KAZI NA HIVYO KUSABABISHA KUVUNJIKA MOYO KATIKA KUHABARISHA UMMA MATUKIO YANAYOJIRI KATIKA JAMII.
WALISEMA KUWA BAADHI YA WANASIASA, JESHI LA POLISI NA WANANCHI WA KAWAIDA WAMEKUWA KIKWAZO KATIKA UTENDAJI WA KAZI AMBAPO WAMETAKA KUWEPO NA MAREKEBISHO YA UPATIKANAJI WA TAARIFA KUTOKANA NA UKIRITIMBA KWA HABARI ZA JESHI LA MAGEREZA, USALAMA WA TAIFA NA MAHAKAMA.
Post a Comment