JUMUIYA ya Waislamu wa Ahmadiya
nchini imesema kuwa sababu za machafuko katika nchi za Mashariki ya Kati
ambako asilimia kubwa ni waislamu zimetokana na waislamu kutofuata kwa
vitendo muongozo wa Koran Tukufu na Hadithi sahihi za Mtume Muhammad (SAW).
Kauli hiyo imetolewa na kiongozi
mkuu wa Jumuiya ya Ahmadiya nchini Amir Tahir Mahmood Chaundry mara
alipowasili Jijini Mbeya kwa ajili ya ziara ya Mkutano wa Amani inayofanyika
Jijini hapa.
Amir Chaundry alisema kuwa mchango
wa Uislamu katika amani ya nchi na dunia ni mkubwa na kwamba machafuko
yanayoendelea katika nchi nyingi zenye waislamu wengi zinatyyokana na
waislamu wenyewe kutofuata maagizo yanayofundishwa katika Kitabu kitukufu cha
Koran.
Akijibu swali kuhusu wajibu wa
Jumuiya hiyo katika kusimamia amani duniani ilhali nchi nyingi za kiislamu
zina machafuko, Kiongozi huyo wa ngazi ya juu katika Jumuiya ya Ahmadiya
nchini alisema, wajibu wa waislamu ni kutii sheria na kufuata maamrisho ya
Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Alibainisha kwa kusema kuwa hali
inayotokea katika nchi nyingi ikiwemo nchi aliyotokea ya Afghanistan
imetokana na kuwepo kwa waislamu wasiojua vyema uislamu.
Alisema kuwa waislamu wengi wako
kwa majina lakini hawatekelezi Uislamu kama unavyoagizwa na Mwenyezi Mungu na
kuwa Jumuiya ya Ahmadiya kwa nafasi yake imejitahidi kutangaza amani na
utulivu duniani kote kwa njia za midahalo,makongamano ya kidini, mikutano na
kusambaza vipeperushi.
Akinukuu baadhi ya aya za Koran
Amir Chaundry alisema kuwa Jumuiya ya Ahmadiya inaamini kuwa kila mtu
ana uhuru wa kuabudu mahala atakako bila kushurutishwa na mtu yoyote.
''Utaona katika nchi za Kiislamu,
Waislamu kwa waislamu wanauana wenyewe kwa wenyewe, hawa ni waislamu lakini
hawaujui Uislamu, tukiusoma vyema Uislamu hakuna vurugu inayoweza
kutokea,''alisema Amir Chandry.
|
Post a Comment
Post a Comment