Mpambano
kati ya timu mbili za ligi kuu Yanga ya Dar es salaam na Mbeya City ya Mbeya
umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.Mchezo huo ambao ulitawaliwa
na shamrashamra na hoihoi uwanja mzima ulikuwa ni wa vuta nikuvute ambapo
hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimetoka uwanjani suluhu bila ya kufungana.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikitaka kupata bao la kuongoza,
bahati iliwaangukia timua Mbeya City mnamo dakika ya 45 ambapo mchezaji
Mwagane Yeya alitumia udhaifu wa walinzi wa timu ya Yanga na kufanikiwa
kuipatia timu yake bao ambalo lilifungwa kwa kichwa na kumuacha golikipa wa
timu ya Yanga Ali Mustafa Baltez akigaa gaa pembeni huku mpira ukiwa umetinga
wavuni.
Mara
baada ya bao hilo la Mbeya City Yanga ilianza kulishambulia lango la Mbeya
City kwa kasi kubwa na kusababisha dakika ya 65 golikipa wa timu Mbeya City
kuutema mpira ambapo mshambuliaji wa Yanga Jerry Tegete aliusukumia wavuni
lakini goli hilo lilikataliwa na mwamuzi Andrew Shamba.
Mnamo
dakika ya 71 Yanga ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia mchezaji
Didier Kavumbagu ambaye aliwatoka walinzi wa timu ya Mbeya City na
kutumbukiza bao kimiani,hadi kipyenga kinapulizwa mabao yalikuwa sare ya 1-1.
Awali
mchezo huo ulitawaliwa na vituko na vurugu za hapa na pale ambapo kabla ya
mechi hiyo kuanza wakati wachezaji wa timu ya Yanga wanaingia uwanjani na
Basi lao kundi la mashabiki wa timu ya Mbeya City walianza kuvurumisha mawe
na chupa na kusababisha Basi hilo kuvunjwa kioo cha upande wa dereva Maulid
Kiula na kumjeruhi mkono wake wa kulia.
Aidha
kituko kingine kilichotokea kabla ya mchezo huo kuanza ni kukutwa mayai
matatu yaliyochorwachorwa katikati ya uwanja ambapo Meneja wa uwanja huo
Modestus Mwaruka aliyaondoa na kuyapeleka ofisini.
|
soka katika mazingira haya haliwezi kutupeleka mbali.Tujirekebishe
ReplyDelete