Kikosi cha timu ya Mbeya City kinachotarajia kupambana na Dar Young African katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine kesho alasiri |
Kikosi cha Timu ya Yanga ambacho kinatarajia kuchuana na timu ya Mbeya City katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kesho alasiri |
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo akizungumza na wanahabari kuhusu mkakati wake wa kuisaidia Mbeya Ishinde katika michezo ya ligi ya Soka. |
Joto la mchezo wa ligi kuu kati ya Timu za Mbeya City na Yanga ya Dar es salaam limeendelea kupanda huku kila upande ukiweka mbinu mbalimbali za ushindi kukabiliana na mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine kesho alasiri
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songwe mkoani Mbeya ameahidi kitita cha sh. milioni mbili iwapo timu ya Mbeya City itaishinda timu ya Yanga ya Jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari jioni hii Waziri Mulugo alisema kuwa mkakato wake ni kuhakikisha kuwa kila timu itakayowasili mkoani Mbeya inaondoka na kipigo katika michuano ya ligi inayoendelea.
Alisema kuwa amedhamiria kuhakikisha timu za Mbeya zinazoshiriki ligi Kuu za Mbeya City na Prison na timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza Kimondo ya Mbozi zote zinapata ushindi mkubwa katika michezo mkoani Mbeya.
''Mbeya City ikiibuka na ushindi nitatoa milioni mbili taslimu kuipongeza, timu ya Prison nayo ikishinda nitatoa shilingi milioni mbili taslimu, nataka timu hizi ziwe mfano na nitahakikisha timu ya Kimondo nayo inapata mafanikio ili mwakani icheze ligi kuu,''alisema.
Alisema kuwa dhamira yake ni kuona mkoa wa Mbeya ambao una vipaji vingi vya michezo kuwa katika ramani ya michezo kitaifa na katika dunia na kwamba kwa kutumia nafasi yake kama kiongozi wa serikali atahakikisha timu zote zinazokuja kucheza na timu za Mbeya zinafungwa.
Post a Comment