Ads (728x90)

SIKU ya mwisho ya Mafunzo kutoka kushoto ni Danny Tweve, Mnaku Mbani(Mwalimu na mwezeshaji) na Rashid Mkwinda (Mmoja wa Waandishi wa Blog hii)

Focus imekaa vyema!! mwanga unatosha ngoja nifotoe kama picha inakuwa bombaa fotoooo!!!!
Aaaa kumbe picha nzuri iko bomba ngoja nirekebishe mwanga kidogo fotoooooo!!!!

Aaaa hapana  hii imesheki kidogo halafu kama iko Out Of focus hebu niendelee kujaribu....Fotooooo!!!!

Nooo!!! bado kidogo, lakini ngoja niendelee kidogo!!! Huyu ni Katibu Tawala Msaidizi Leornad Magacha akitoa ufafanuzi juu ya fursa za kiuchumi zilizopo mkoani Mbeya mbele ya waandishi wa habari




 SONGWE INTERNATIONAL AIR PORT(SIA)

BAADA ya kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Msaidizi safari iliendelea hadi Songwe International Air Port(SIA)
Wanahabari waliwasili na kukaa kwa takribani nusu saa kabla hawajaingia uwanjani na baadaye kuingia na kupekuliwa kabla ya kuingia katika maeneo mbali mbali ya Uwanja wa Songwe

Wanahabari wakiongozwa na Ofisa Mwendeshaji wa Viwanja vya Ndege Patania Kyoomo ambaye aliwatembeza maeneo mbalimbali ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe







Mchumi wa Mkoa wa Mbeya Rukia Manduta akitoa ufafanuzi juu ya fursa za uwekezaji zilizopo katika mkoa wa Mbeya mbele ya waandishi wa habari walitembelea ofisini kwake.

























JIONI
Mara baada ya kumaliza mizunguko yote ya mchana kutwa na kumaliza mafunzo jioni walipata fursa ya kuketi pamoja na kubadilishana mawazo huku wakiburudika kwa vinywaji na chakula, hii ni get together iliyofanyika katika ukumbi wa City Pub, waandishi waliendelea kupata vinywaji na chakula kwa takribani saa nzima lakini baadaye Uongozi wa Pub hiyo uliwaingiza nyongo wanahabari pale walipoombwa kuweka taarifa ya habari ilipofika saa 2:00 kamili na uongozi huo kukataa kufanya hivyo.



Kilichofuatia baada ya hapo ni wanahabari kuamua kuondoka eneo hilo huku wakikosa ladha halisi ya taaluma yao ya kuangalia taarifa ya habari na hivyo kuonesha namna ambavyo wamiliki wengi wa Pub na Bar wa Jijini Mbeya wasivyothamini umuhimu wa habari ambazo zinawasaidia aidha kujua mambo taarifa mbalimbali zinazotokea ndani na nje ya nchi.

Na,Bloga Wetu Mbeya
ASILIMIA 40 ya mapato ya Mkoa wa Mbeya yanatokana na shughuli za kiuchumi katika sekta za viwanda,biashara na kilimo huku asilimia 80 ya wakazi wake wakijishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara.
Akizungumza na timu ya waandishi wa habari waliokuwa katika mafunzo ya habari za Biashara na Uchumi mkoa wa Mbeya, Mchumi wa mkoa Bi. Rukia Manduta alisema asilimia 40 ya mapato hayo yanatokana na uwekezaji katika Viwanda,Madini, Biashara na usafirishaji.
Alisema kuwa serikali inaendelea kuimarisha miundo mbinu katika barabara ambapo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe umeongeza chachu kwa wakulima kupata fursa ya kusafirisha mazao ya kilimo kama vile maua mbogamboga na matunda.
Aidha alisema kuwa uwekezaji katika sekta ya utalii umeendelea kuimarika kwa Bonde la Ihefu lililopo wilayani Mbarali kuingizwa katika Hifadhi ya Taifa ilhali Ziwa Rukwa lililopo  wilayani Mbozi na Chunya na Ziwa Nyasa lililopo katika wilaya ya Kyela yanasaidia pato la mkoa katika sekta ya usafirishaji na uvuvi.
Kwa upande wake Ofisa Biashara wa mkoa wa Mbeya Bw. Joseph Semu alizitaja baadhi ya changamoto zinazochangia kukosekana kwa wawekezaji wakubw kuwa ni pamoja na uhaba wa maeneo na kwamba kufuatia hali hiyo Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro ameunda timu ya watu sita ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
Bw. Semu alisema kuwa timu iliyoundwa na Mkuu wa mkoa imechukua wataalamu kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo mkoa wa Mbeya(SIDO),TCCIA,TIC, Mhadhiri wa chuo kikuu Mzumbe, na wataalamu wawili kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa.
Awali akizungumza na Katibu Tawala msaidizi wa mkoa wa Mbeya Bw. Leonard Magacha, mkufunzi wa mafunzo ya habari za Biashara na Uchumi kwa waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Bw. Mnaku Mbani alisema kuwa lengo la mafunzo hayo kwa wanahabari ni kuwajengea uwezo wanahabari kuandika habari za biashara na uchumi.
Alisema fursa hiyo kwa wanahabari imelenga kuibua changamoto za kiuchumi kwa mkoa wa Mbeya kwa nia ya kupatiwa ufumbuzi na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo mkoani humo.
Naye Katibu tawala Msaidizi mkoa wa Mbeya Bw. Magacha alisema kuwa mkoa umeunda na kuzindua mabaraza ya biashara kwa halmashauri za wilaya ambayo yataimarishwa  kwa nia ya kuboresha usambazaji wa huduma za kijamii kama vile elimu, afya na maji.
Alisema kuwa matarajio ni kufanya mkutano wa Jukwaa la wawekezaji mkoani humo ambapo wawekezaji mbalimbali  watapata fursa ya kuutembelea mkoa na kuona aina ya uwekezaji unaofaa.

Post a Comment