Ads (728x90)

Katika hali isiyo ya kawaida mwanadada huyu alikutwa na kamera yetu mitaa ya Jijini Dar es salaam akihaha na mwanambuzi mgongoni huku mwanambuzi huyo akiliaaa meeee!!!!


Mwanadada huyo alilazimika kumbembeleza mwanambuzi huyo aliyekuwa akilia kwa sauti kiasi cha kuwashangaza wapita njia, jamaa mmoja alisikika akisema kuwa, Mwanambuzi Meee amlilima mamaye!!!



Kuna wakati mwanambuzi huyo alitaka kuchoropoka katika mbeleko ya mwanadada huyo lakini mwanadada huyo alijitahidi kuifunga vyema mbeleko yake ili mwanambuzi huyo akae vyema, haikufahamika mara moja mwanadada huyo alikuwa akimpeleka wapi mwanambuzi huyo ambaye alionesha wazi kuwa alikuwa akimlilia mamaye ili anyonye!!!, Makubwa ya mjini!!!!


Post a Comment

Post a Comment