Kikosi cha timu ya Stendi ambacho kilichuana na timu ya Prison na kufungwa mabao 3-0 |
Benchi la Prison likiwa na baadhi ya wachezaji wa akiba wa timu hiyo |
b
Kocha wa Prison Mbwana Makata akizungumzia hali ya mchezo baada ya kumalizika kwa |
NI magoli
3-0 ya timu ya Tanzania Prison ya Jijini Mbeya inayomilikiwa na Jeshi la
Magereza nchini dhidi ya Wapiga Debe wa Shinyanga Stand Unite, yameisaidia timu
hiyo angalau kuwa na matumaini ya kuendelea kubaki katika Ligi Kuu iwapo
wataendelea na ushindi kwa mechi zilizosalia.
Hata hivyo
ushindi huo wa kimbunga dhidi ya timu ngeni katika ligi hiyo Stand bado
unaibakisha timu hiyo katika nafasi ya mkiani ikiwa imejitwalia juma point 16
dhidi ya point 13 ilizokuwa nazo awali.
Ushindi huo
wa Prison umetoa tafsiri halisi ya maamuzi magumu yaliyofanywa na timu hiyo ya
kumtema aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo David Mwamwaja na mikoba yake
kurithiwa na Mbwana Makata ambaye amewakiwa na nyota njema ya ushindi wa
kimbunga.
Ushindi wa
Prison ulianza kuonekana dakika za mwanzo za mchezo huo ambapo vijana hao
tofauti na ilivyokuwa katika michezo mingine walionekana kujituma na kucheza
kwa ari kubwa ya kuhitaji ushindi.
Wasambuliaji
wa Prison akina Jeremia Juma Jimmy Shoji,Amir Omar na Hamisi Maingo walionekana
ni mwiba mchungu kwa walinzi wa Stendi akina Abuu Ubwa, Jisendi Maganda,Peter
Mutabuzi na Reyna Mgungira.
Golikipa wa
timu ya Stend John Mwenda alikuwa na kibarua kizito cha mashambulizi kutoka kwa
washambuliaji wa Prison ambao walionekana kucheza bila kuchoka kutoka mwanzo
mwa mchezo hadi mwisho.
Mashambulizi
hayo ya mara kwa mara katika goli la Stendi yalizaa matunda katika dakika 30 ya
mchezo ambapo Beki wa Prison Laurian Mpalile alipoipatia timu yake bao la
kwanza baada ya kuwatoka walinzi wa Stendi na kumimina shuti kali lililomwacha
golikipa wa Stendi John Mwenda akichupa bila mafanikio.
Goli hilo
liliamsha hamasa kwa wachezaji wa Prison na kucheza kwa kuonana vyema huku
wachezaji wa Stendi ambao wanaonekana kama bado hawajaizoea mikiki mikiki ya
ligi hii wakipigiana pasi mbovu na mipira kuwafikia wachezaji wa Prison.
Hata hivyo
almanusura mashabiki wa timu hiyo kongwe katika ligi hiyo waingie nyongo kwa
kujifunga wenyewe baada ya mchezaji wake Salum Kimenya kupiga tiktaka iliyokatwa
na upepo na kuelekea golini kwake ambapo hata hivyo golikipa Mohamed Yusuf
wa Prison alipangua mpira huo uliopita
juu ya mwamba na kusababisha kona.
Mashambulizi
ya uchu wa kupata magoli ya Prison yaliendelezwa kwa kasi kubwa na kusababisha
dakika ya 41 Amir Omar kuwatoka walinzi wa Stend na kubaki na golikipa John
Mwenda na kuukwamisha mpira nyavuni lakini mshika kibendera wa upande wa
mashari ya uwanja alinyoosha kibendera cha kuotea kwa mchezaji huyo.
Hadi filimbi
ya mapumziko inapulizwa Prison walitoka kifua mbele kwa goli 1 -0.
Kipindi cha
pili kilianza kwa kasi kubwa kwa wachezaji wa Prison kuonesha kandanda safi
huku wachezaji wa Stend wakihaha kusawazisha bao bila mafanikio.
Ilikuwa ni
timu ya Prison tena mnamo dakika ya 52 ya mchezo ambapo mara hii mchezaji
Hamisi Maingo aliwainua mashabiki wa timu hiyo kwenye viti kwa kushangilia
baada ya kuopachika bao maridadi lililotokana na pasi ya mshambuliaji mrefu
Ibrahimu Is- haka.
Maingo mara
baada ya kupokea pasi kutoka kwa Is haka aliwalamba chenga walinzi wa Stend
Jisendi Maganda,Abuu Ubwa na Peter Mutabuzi na baadaye kumlamba chenga golikipa
na kutingisha wavu na kulifanya ni goli la 2 kwa Prison.
Kama vile
haikutarajiwa mashabiki waliozoeleka kutoishangilia timu ya Prison ambao mara
nyingi huketi katika jukwaa la kaskazini waliinuka vitini na kushangilia goli
hilo na hivyo kurejesha uhai kutokana na uhasama mkubwa uliopo baina yao
wanafamilia wa timu hizo mbili.
Bao hilo
lilizidi kuwachanganya wachezaji wa timu ya Stendi United yenye kawaida ya kuwa
na mashabiki wenye vurugu kubwa uwanjani wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani
na hivyo kuonekana kama walionywea na kuloa maji ya baridi.
Kuchanganyikiwa
kwa wachezaji hao kuliendelea kuamsha ari kwa wachezaji wa Prison ambao
walilishambulia goli la United kama nyuki na kusababisha msukosuko katika lango
lao na hivyo kusababisha kona katika dakika ya 60.
Kona hiyo
iliyochongwa kiufundi na Jeremiah Juma
ilitua katika kichwa cha Hamis Maingo ambaye bila ajizi aliruka kama Nyani na
kupiga m;pira huo kwa kichwa na mpira kutinga wavuni na kumwacha golikipa na
walinzi wa Stend wakishindwa kuamini macho yao.
Baada ya
kuingia kwa goli hilo wachezaji wa Shinyanga walionekana kukata tamaa huku
wakiwa wamechoka kupita kiasi ilhali wenzao wa Prison wakizidi kuongeza kasi
wakihitaji kuongeza bao la 4.
Hadi
kipyenga cha mwisho kinapulizwa Prison walikuwa kifua mbele kwa goli 3 didi ya
0 ya Stendi United.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo kocha mpya wa Prison Mbwana Makata
alisema kuwa, amejitahidi kuwatyuni kisaikolojia wachezaji wake na kuwajengea
uwezo mpya katika kukabiliana na janga la kushuka daraja kwa timu yao.
Kwa upande
wake Kocha wa United Mathias Lule mbali na kukubali kushindwa katika mchezo huo
alitupia lawama waamuzi(bila kufafanua zaidi) kwamba walikuwa wakichezesha mpira
kwa upendeleo.
Timu ya
Stendi inaelezwa itaendelea kubaki Jijini Mbeya ikisubiri mechi yake Mbeya City
inayitarajiwa kupigwa katika dimba hilo Jumatano ijayo, huku Mbeya City wakiwa
wanatarajia kukabiliwa na kibarua kigumu katika mchezo wake kesho
atakapokumbana na Maafande wa Tanga Mgambo Shooting.
We From SEO Milanisti Introduces Its Sales Sells Herbal Products Men And Women ALL PRODUCTS FROM our clients in Down's.
ReplyDeletepembesar penis | obat pembesar penis
parfum pemikat wanita | perangsang wanita