Ads (728x90)


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akikabidhiwa Tuzo maalum ya kusimamia Amani katika mkoa wa Mbeya kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Maimamu wa mkoa wa Mbeya Sheikh Idd Tuwa wakati wa kikao maalum cha kuzungumzia Amani Mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa katika kikao maalum cha kuzungumzia amani mkoa wa Mbeya leo asubuhi.
 




Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akizungumza na viongozi wa dini ya kiislamu kwenye ukumbi wa Mkapa leo asubuhi.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwausia waislamu kwenye kikao maalum cha kuzungumzia amani mkoa wa Mbeya.

Baadhi ya akina mama wa Kiislamu wakiwa katika kikao cha amani mkoa wa Mbeya leo asubuhi.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akipokea Tuzo ya kusimamia Amani mkoa wa Mbeya kutoka Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu Tanzania (TAMSYA)Shekhe Nassor Abdallah ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wake katika kudumisha amani mkoa wa Mbeya..

Baadhi ya Viongozi wa Kiislamu wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro mara baada ya kikao cha kuzungumzia amani na utulivu wa mkoa wa Mbeya.
MKUU wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewaondoa hofu viongozi wa dini ya Kiislamu na waumini wao kwa kusema kuwa kitendo cha kufuga ndevu na kufanya ibada havina uhusiano wowote na dhana ya ugaidi.
Kandoro aliyasema hayo leo asubuhi katika kikao maalumu cha kuzungumzia Amani na Utulivu mkoani Mbeya ambacho kiliratibiwa na Umoja wa Maimamu na kufanyika katika ukumbi wa Mkapa.
''Hakuna Uhusiano wowote kuhusu ufugaji wa ndevu na mambo ya ugaidi,..si wote wanaofuga ndevu na kufanya ibada ni magaidi, ugaidi ni kitendo cha mtu hakihusiani kabisa na Uislamu''alisema.
Alisema kuwa Uislamu ni dini inayofundisha amani na utulivu na wanaoifuata dini hiyo hufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kuwa kitendo chochote cha ugaidi kinachofanywa na baadhi ya watu hakihusiani na Uislamu.
Awali akizungumza katika kikao hicho kilichowakutanisha viongozi wa dini na waumini ya Kiislamu mkoani Mbeya, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema kuwa waislamu wanapaswa kuepuka migogogoro miongoni mwao ili kujenga amani na utulivu katika jamii.

Post a Comment