Ads (728x90)

Hatimaye safari ya zaidi ya km 800 iliyochukua takriban siku 8 imekamilika kwa wapanda baiskeli watatu vijana kutokea Jijini Mbeya kuwasili Jijini Dar es salaam na kukutana na Mkuu wa mkoa huo Said Meck Sadick
 .

Vijana hao walkioanza safari yao Jumatatu iliyopita walipita mikoa minne ya Njombe, Iringa, Morogoro, Pwani na hatimaye kuingia Jijini Dar es salaam huku wakikumbana na changamoto mbalimbali barabarani lakini hatimaye makusidio yao yamekaribia kutimia kwa kukutana na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ambaye atafanya mpango wa kuwakutanisha na Rais Jakaya Kikwete ambao watamkabidhi ujumbe maalum uliopo katika kitabu chao.
  
Lemgo la safari yao ambayo imeambatana na ujumbe wa kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kutimiza miaka 10 kwa mafanikio lilikuwa pia ni kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura ambapo walitoa elimu hiyo katika vijiji mbalimbali walivyopita katika safari yao.
Kiongozi wa wapanda Baiskeli kutoka Jijini Mbeya Wizeman Luvanda akkiongoza msafara wa wenzie watatu wakiwasiri Jijini Dar es salaam baada ya safari iliyowachukua takriban siku 8 kutokea Jijini Mbeya. 
Pichani mmoja wa wapanda baiskeli kutokea mkoani Mbeya akitoa burudani katika kijiji cha Mlandizi walipokuwa njiani kuelekea Jijini Dar es salaam kwa baiskeli.

Post a Comment