| Maisha ni kuhangaika maisha ni kutafuta hata watoto nao wanahangaika na maisha katika kipindi cha likizo wakitafuta fedha za kujikimu mara ifunguapo shule. |
| Mtoto huyu anaokekana akiwa na maparachichi kichwani akitafuta wateja,huamka asubuhi na kuzunguka mjini hadi jioni ili angalau aweze kujipatia senti za kujisaidia. |
| Naye mtoto huyu kama alivyo yule anayeuza mapapai anajikimu kwa kuuza ndizi mitaani kila siku ili hatimaye siku inapofunguliwa shule amudu kujinunulia madaftari. |
| Mtoto huyu naye hakuwa nyuma katika kujitafutia riziki alionekana akiuza mahindi mabichi mitaani. |
| Naye huyu alikutwa na mwanablog wetu akihaha mitaani akijitafutia riziki kwa kuuza maparachichi |
Post a Comment