Ads (728x90)

Watu wasiofahamika wamevamia na kuingia katika nyumba ya Mwandishi wa habari wa kampuni ya IPP Media mkoani Mbeya Thobias Mwanakatwe, na kuiba mali yenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 4.


Mwanakatwe amekumbwa na mkasa huo wakati akiwa safarini wilayani Rungwe ambako alikuwa katika majukumu yake ya kazi za kila siku.


Akizungumza na MWANAFASIHI alisema kuwa watu hao walivamia usiku wa Disemba 24 na kuchukua Tv mbili zenye ukubwa wa inch 21,Redio kubwa aina ya Sub ufa, Kompyuta moja,Deki, Receiver,Jiko la Umeme,Jiko la Gesi, Mtungi wa gesi, Mikoba sita ya wanawake,suti za kike na kiume pamoja na nguo zingine ambazo zote zina thamani ya sh. 4,037,000/-

Alisema kuwa alipigiwa simu na jirani yake nyumbani anakoishi mtaa Majengo mtaa wa Hiari ya Moyo kwamba nyumba anayoishi imevunjwa na kuibiwa kila kitu ambapo mara alipofika alienda kutoa taarifa katika kituo cha polisi cha Stendi Kuu na kupewa hati namba STKUU/MB895/2011.

(Mwanakatwe akizongwa na askari polisi katika moja ya harakati zake za kiuandishi wakati akitekeleza wajibu wake na kujikuta na askari wa Usalama Barabarani )

Mwanakatwe akitoka kituo cha Polisi centro jijini Mbeya ambako alishikiliwa na polisi kutokana na kutofautiana katika utendaji wa kazi
Mwanakatwe amekuwa ni miongoni mwa waandishi wa habari wanaofuatilia kwa kina habari za kijamii na zile ambazo zinagusa maslahi ya watu bila kujali cheo wala wadhifa wa anayehusika ambapo mara kadhaa amekuwa akikumbwa na vitisho ikiwemo kushikiliwa na polisi.

Akizungumza kama tukio hilo linaweza kushabihiana na shughuli zake za kiuandishi, alisema kuwa hana uhakika na hilo ingawa pia linaweza kuwa linahusiana na kazi zake anazozifanya kwa kuwa zinagusa maslahi ya watu.

MWANAFASIHI:Inawezekana kuwa tukio hili la wizi linashabihiana na kazi zako za uandishi unazofanya?

MWANAKATWE: Sina uhakika na hilo lakini inawezekana kuhusishwa na kazi yangu...si unajua tena hizi kazi zetu zinazalisha maadui wengi?

Post a Comment