Sakata la mawipii na makonstebo wa polisi wanne wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Mbozi kuhusishwa na njama za kuwatorosha watuhumiwa wa wizi wa gari baada ya kuhongwa kiasi cha sh.milioni 2,limegubikwa na utusiutusi ndani ya jeshi hilo huku askari hao wakiwa wamevuliwa magwanda meupe na kusubiri hatima yao.
Tukio hilo ambalo limekuwa gumzo miongoni mwa askari wa usalama barabarani mkoani Mbeya linaelezwa kuwakumba watu wasiokuwamo huku likielezwa kuwa waliolamba mshiko huo wanakula kuku pamoja na kuvuliwa magwanda meupe na kubaki nje ya ulingo huku upelelezi ukiendelea.
Askari wanaodaiwa kulamba mshiko huo na kuwaingiza wenzao mkenge wanaonekana wakivinjari mitaani maeneo ya Mlowo na Vwawa wilayani Mbozi huku wakijipongeza na kupongezwa na baadhi ya watu na kuonekana kama mashujaa kwa kuwaingiza wasiokuwemo katika tukio hilo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ni kwamba askari hao wa jinsi ya kike ambao ndio wanaodaiwa kulamba mshiko huo wamekuwa katika furaha ya aina yake wakisubiri kusherehekea xmass na mwaka mpya huku wenzao wa kiume ambao wameambulia msala huo wakitafakari hatima yao juu ya msala walioambukizwa na mademu hao wavaa magwanda meupe.
‘’Hawa mademu hawana hata wasiwasi si unawaona wakivinjari mitaani na gari lao, wanafurahia wenzao kuingizwa katika mkenge pamoja,’’alisema mmoja wa watoa taarifa bila kutajwa jina lake.
Naye askari mmoja ambaye pia hakupenda kutajwa jina lake kutokana na kuwa si msemaji alisema kuwa,askari hao wa kike ndio tabia yao na kuwa siku hiyo ilifika arobaini yao bali hata hivyo wamewaambukiza wenzao ambao hawakuwa wanajua lolote juu ya tukio hilo la wizi wa gari.
Juzi blogi hii imeripoti juu ya tukio la uporaji wa gari aina ya Toyota Ipsum lenye namba za kubandikwa T 173 BKT ambalo awali lilikuwa na namba za IT linalodaiwa kuibiwa bandarini Jijini Dar es salaam.
Kubambwa kwa gari hilo kulitokana na askari wawili wa kiume kulitilia mashaka gari hilo ambapo mara baada ya kulisimamisha askari wa kike walifika eneo la tukio la kuwapiga mkwara askari wenzao wa kiume na kuanza mzozo ambapo baadaye mmoja wa askari wa kike anadaiwa kumbonyeza mmoja wa watuhumiwa aingie mitini ili kupoteza ushahidi.
‘’Hawa mademu ni soo wamewaingiza mkenge jamaa,wamelamba mshiko halafu wameuchuna,hiyo hela itawatokea puani wale njemba wawili hawajui kinachoendelea juu ya mshiko,’’alisema jamaa mmoja mkazi wa mjini Vwawa ambaye anafahamu vyema sakata hili lilivyokuwa.
Taarifa zilidai kuwa askari hao walifika eneo hilo baada ya kupigiwa simu na watuhumiwa hao ambao awali walikutana na akina dada hao na kuwakeshi Milioni Mbili za Kitz ili kuua soo waliyokuwa nayo ya wizi wa gari.
Inaelezwa kuwa katika sekeseke hilo askari wa kiume walishangazwa na kitendo cha askari hao wa kike kuvalia njuga suala hilo ambapo hata hivyo wakiwa katika taharuki walitokea askari wengine ambao walilisindikiza gari hilo hadi Centro Polisi Jijini Mbeya huku akina dada hao wakirejea Vwawa.
Aidha inaelezwa kuwa mara baada ya kuibuka kwa sakata hilo watuhumiwa hao wote walifikishwa kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi ambaye aliwaketisha chini na kuwahoji kwa undani juu ya tukio hilo ambapo mara baada ya maelezo yao walivuliwa magwanda na kutakiwa kukaa benchi hadi uchunguzi utakapokamilika.
END…..
Post a Comment