UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU
ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT.
JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda (Mb.,) kutokana na kifo cha Mhe.
Jeremia Solomon Sumari, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa
tiketi ya CCM na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, kilichotokea usiku wa kuamkia
leo tarehe 19 Januari, 2012 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa
amelazwa kwa matibabu.
“Nimeshtushwa,
nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha Mheshimiwa
Jeremia Solomon Sumari kwani alikuwa kiongozi aliyewatumikia vema wananchi wa
Jimbo lake la Uchaguzi la Arumeru Mashariki na Taifa kwa ujumla katika wadhfa
wake wa Waziri kwa umahiri na uhodari mkubwa”, amesema Rais Kikwete katika
salamu zake.
Rais
Kikwete amesema kutokana na kifo chake, wananchi wa Arumeru Mashariki
wamepoteza kiongozi wa kutegemewa sana huku Taifa likiachwa na pengo kubwa
ambalo si rahisi kuzibika ikizingatiwa kwamba alikuwa kiongozi katika Wizara
ambayo ni mhimili muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.
“Kwa
dhati ya moyo wangu, natuma salamu za rambirambi na pole nyingi kwa familia ya
Marehemu Jeremia Sumari kwa kumpoteza kiongozi na mhimili madhubuti wa
familia. Ninawahakikishia kwamba nipo pamoja nanyi katika kuomboleza
msiba huu mkubwa, na namuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema aipumzishe roho
ya Marehemu Jeremia Solomon Sumari mahali pema peponi, Amina”, ameongeza kusema
Rais Kikwete.
Ameiomba
familia ya Marehemu kuwa na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki
kigumu cha maombolezo ya mpendwa wao kwa kutambua kuwa yote ni mapenzi yake
Mola.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
19
Januari, 2012
Post a Comment