|
MADIWANI 24 wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
wanafanya ziara ya siku nne wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya kwa nia ya
kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo,utoaji huduma za kiafya CHF,Masjala
ya ardhi na mafanikio ya ukusanyaji wa kodi kwa ngazi za vijiji, mitaa
na wilaya.
Akizungumza
kwa njia ya simu juu ya ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Namtumbo Bw. Mussa Zungiza(pichani juu) alisema kuwa ziara hiyo itaongozwa na
Mwenyekiti wa Halmashauri Bw. Stephan Nana ambayo italenga kujifunza
mafanikio mbalimbali ambayo halmashauri ya wilaya Mbozi imeyapata
kutokana na kujali utawala bora kati ya wananchi na watendaji wa
serikali.
Bw. Zungiza alisema kuwa halmashauri
ya wilaya ya Namtumbo ina fursa nyingi za kiuchumi
zikiwemo zile zitokanazo na mazao ya biashara na chakula kama vile
Tumbaku,Korosho,Ufuta, Alizeti na mazao ya chakula ambayo ni mahindi na
mpunga ambayo iwapo wananchi wakiyatumia vyema wanaweza kujikwamua
kiuchumi na kuondokana na umaskini.
|
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmaashauri ya Wilaya ya Mbozi Levison Chillewa |
| | |
| | ''Wilaya
hizi zinafanana kwa kila hali kuanzia mazao yanayolimwa. jiografia
yake... ni muhimu kujua mbinu mbadala za uzoefu ili kuboresha huduma za
kijamii na kiuchumi ndani ya halmashauri yetu,''alisema.
''Tumezingatia
mafanikio ya Mbozi katika maeneo mengi
..kama vile ukusanyaji kodi kwa
ngazi za vijiji, kata na wilaya, uundwaji wa miji midogo, hati miliki za
kimila ambazo wananchi wanakopesheka kutokana na ardhi yao ya
asili,''alisema Bw. Zungiza.
Alifafanua kuwa
Wilaya ya Mbozi imefanikiwa katika usimamizi wa miradi kutoka ngazi za
kata na vijiji jambo ambalo linaonesha kuna ushirikishwaji mkubwa baina
ya watendaji wa serikali na wananchi.
Bw.
Zungiza alisema kuwa ziara hiyo inaanza leo na kukamilika Januari 20
ambapo ambapo pia madiwani hao watapata fursa ya kutembelea wilaya ya
Njombe iliyoko mkoani Iringa ambakoina mandhari na jiografia
inayoshabihiana na wilaya ya Namtumbo.
''Wilaya
hizi zinafanana kwa kila hali kuanzia mazao yanayolimwa. jiografia
yake... ni muhimu kujua mbinu mbadala za uzoefu ili kuboresha huduma za
kijamii na kiuchumi ndani ya halmashauri yetu,''alisema.
|
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bw.Levison
Chilewa alisema kuwa, mafanikio ya Halmashauri hiyo yanatokana na
ushirikishwaji uliopo baina ya watendaji wa serikali na wananchi ambapo
hamasa kubwa imetokana na wananchi kukubali kuhudhuria mikutano ya
vijiji na kata na kwamba viongozi wa serikali wamehimizwa kuwa na
utaratibu wa usomaji wa mapato na matumizi kwa wananchi.
Post a Comment