Ads (728x90)



Na, Rashid Mkwinda
ZIKIWA zimepita siku nne tangu watu 11 kufa katika ajali iliyohusisha magari matatu likiwemo gari la Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya Dkt. Mary Mwanjelwa, watu wengine 20 wamenusurika kufa katika ajali iliyotokea eneo la Mafiat katikati ya Jiji la Mbeya.

Ajali hiyo imehusisha magari mawili aina Pick Up Double Cabin Ford Ranger yenye namba za usajili T 189 BLP iliyokuwa ikielekea upande Mwaanjelwa ikitokea mjini na Hiace iliyokuwa ikielekea TAZARA ambapo magari hayo yalijikuta yakigongana uso kwa uso kiasi cha kuwajengea hofu abiria waliokuwemo ndani ya Hiace.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ni kwamba gari aina ya Pick Up lilikuwa katika mwendo wa kasi huku Hiace ikikimbilia abiria katika kituo kinachofuata na kwamba hakukuwa na tahadhari kati ya madereva wa magari.






Ajali hiyo nusura iongeze simanzi nyingine baada ya ajali kubwa iliyotokea eneo la Mbalizi na kusababisha vifo vya watu 11 akiwemo Katibu wa Mbunge wa viti maalumu mkoani Mbeya Dkt. Mary Mwanjelwa aliyetambulika kwa jina la Amina Mwashamba ambapo dereva wake Rajab Majuto alivunjika miguu yake mara tatu.

Post a Comment