Ads (728x90)


MSANII maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepata dhamana leo baada ya kukidhi masharti aliyowekewa na mahakama.

Dhamana hiyo imetolewa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya hoja za mawakili wanaomtetea kukubalika.

Masharti aliyokuwa amepewa ni pamoja na wadhamini wawili wafanyakazi wa serikali wenye kiasi cha Sh. milioni 20 kila mmoja na kuwasilisha pasi ya kusafiri ya msanii ili kutotoka nje ya nchi hadi kesi hiyo itakapokamilika.

Huku mashabiki wake na baadhi ya wasnii wenzake wakiwa na furaha mahakamani hapo, kila mmoja alisikika akisema Mungu mkubwa.(CHANZO GLOBAL PUBLISHERS)

 


Post a Comment