Ads (728x90)

Mtia nia wa Ubunge Jimbo la Busokelo Suma Mwakasitu akiweka saini katika kitabu cha Ofisi za CCM Wilaya ya Rungwe leo asubuhi


Bi. Mwakasitu akihesabu mpunga kwa ajili ya kulipia ili kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Ubunge jimbo la Busokelo


Mtia nia wa Ubunge jimbo la Busokelo Bi. Mwakaskitu akimkabidhi fedha taslimu kiasi cha sh.1,100,000 kwa Katibu wa chama wilayani humo Bi.Mariam Yusuf ambazo ni sh. laki moja za fomu ya Ubunge na Sh. milioni moja za kuchangia gharama za kampeni za uchaguzi huo.







Katibu wa CCM Wilaya ya Rungwe Bi. Mariam Yusuf akitoa nasaha








































Bi. Mwakasitu akitoa katika Ofisi za CCM Wilaya ya Rungwe mara baada ya kuchukua fomu za kuwania kuteuliwa kugombea Ubunge jimbo la Busokelo



Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuchukua fomu nje ya Ofisi za CCM Wilaya ya Rungwe








Baadhi ya wanachama wa CCM kutoka jimbo la Busokelo wakiburudika na vinywaji katika hotel ya Landmark iliyopo Tukuyu mjini ambao walifika kumsindikiza mtia nia Bi. Mwakasitu





MWANAMAMA pekee mtia nia wa Ubunge Jimbo la Busokelo,Kamishna Ardhi Msaidizi Kanda ya Pwani Suma Mwakasitu(53) amejitokeza na kuchukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya CCM ambalo awali lilikuwa chini ya Profesa Mark James Mwandosya.
Akizungumza kwa kujiamini na kuonesha nia ya dhati ya kupokea kijiti cha Prof. Mwandosya ambaye aliaga rasmi jimbo hilo baada ya kuweka nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano,Bi. Mwakasitu alisema anawiwa moyoni mwake kuwatumikia wana Busokelo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
‘’Mimi ni mwana Rungwe, ni mkazi wa jimbo la Busokelo nimeona ni vyema nikajitokeza kuchukua fomu ya kuwania Ubunge ili niendeleze pale alipoishia Prof. Mwandosya,’’ alisema.
Alisema jimbo hilo limejengwa na kuachiwa misingi mizuri na aliyekuwa Mbunge wa wake na Waziri wa Ofisi ya Rais Kazi Maalum Prof. Mwandosya na kuwa anahitajika mtu makini kuendeleza pale alipoachia na kuwa anaamini yeye anatosha kumpokea kijiti na kusukuma mbele zaidi maendeleo ya jimbo hilo.
‘’Mimi siku zote huwa naliita jimbo hili kuwa ni Small Paradise kutokana na kuwepo na uoto wa asili wa rangi ya kijani kibichi, ardhi yetu yenye rutuba inastawi kila aina ya mazao, anahitajika mtu makini kusimamia na kuendeleza hayo,’’alisema.
Alisema yeye amekuwa mwanamama pekee aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo ya Ubunge wa jimbo tofauti na akina mama wengine ambao wamejitokeza kuwania Ubunge wa Viti maalum na kuwa ameamini dhamira yake imesukumwa na utashi wake na hamasa ya maendeleo ya Jimbo hilo.
Alibainisha kuwa zipo fursa nyingi ambazo wanawake wanaziweza pamoja na woga walionao wa kuthubutu katika fursa zilizopo.
Aidha Bi. Mwakasitu alisema anatupa karata hiyo kuomba ridhaa ya chama chake kumsimamisha agombee ubunge na kuwa hata kama kura hazitotosha atamuunga mkono mgombea atakayeteuliwa na chama chake.
Kwa upande wake Katibu wa CCM wilayani Rungwe Bi.Mariam Yusuf alisema kuwa wilaya ya Rungwe alisema kuwa wilaya hiyo ina majimbo mawili la Rungwe na Busokelo ambapo hadi sasa jumla ya watia nia 15 wamejitokeza kuomba nafasi za Ubunge kwa majimbo yote mawili.
Alisema kuwa hadi leo asubuhi jimbo la Rungwe walijitokeza wagombea saba ambao ni Kigula Mwambene,Obadia Ndangali,Zacharia Mwansasu,Joel Mwakila, Richard Kasesela, Mfanyabiashara maarufu nchini Sauli Amon maarufu kwa jina la S.H. AMON,na aliyewahi kuwa mbunge wa Kigamboni kwa tiketi ya CUF kabla ya kurejea CCM Frank Magoba.
Kwa upande wa jimbo la Busokelo Bi. Yusuf aliwataja wagombea nane waliojitokeza ambao ni pamoja na Issa Mwakasendo,Ezekiel Mwakyambo,Juma Kaponda,Lusubilo Mwakabibi,Steven Mwakajumilo,Ali Mwakibolwa, Aden Mwakyonde na Bi. Mwakasitu.

Post a Comment