Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipita kwenye eneo la kivuko cha Kibundungulu kilichopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya ambacho kinajengwa |
Mkazi wa kijiji cha Kibundungulu akipita ndani ya mto Mbaka kutokana na kivuko cha eneo hilo kuvunjika baada ya kutokea mafuriko wakati wa masika |
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akishiriki kukoroga zege kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha Kibundungulu wilayani Rungwe |
Mkuu wa mkoa wa Mbeya akizungumza na wakazi wa eneo la mto Mbaka ambako kinajengwa kivuko |
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kivuko katika mto Mbaka wilayani Rungwe |
Kilio cha
wakazi wa kitongoji cha Kibundungulu kilichopo katika kijiji cha Mbaka wilayani
Rungwe waliokuwa wakipata tabu kuvuka kwenye kiteputepu sasa kumalizwa mwezi
ujao.
Mkuu wa mkoa
wa Mbeya Amos Makalla ambaye amewatembelea wananchi wa kitongoji hicho na
kushiriki ujenzi wa kivuko hicho jana amesema kitengo cha Maafa Ofisi ya Waziri
Mkuu TAMISEMI kimemuwezesha Mkandarasi kukamilisha kivuko hicho kwa muda wa
wiki mbili.
Amesema kwa
mujibu wa mkandarasi kivuko hicho kitakamilika Julai 8 na wananchi wa kijiji
hicho wataanza kupata huduma muhimu za kijamii kwa kutumia kivuko hicho.
Awali
wananchi wa maeneo hayo walikuwa wakipita ndani ya mto kutokana na kivuko hicho
kusombwa na maji wakati wa masika na kwamba kivuko hicho kitakuwa ni cha muda
huku kukiwa na mkakati wa kujenga daraja la kudumu.
Aidha
Makalla amewasihi wananchi kuacha kuvuka kwa kutumia waya na kuwa kukamilika
kwa kivuko hicho kitasaidia wananchi kuondokana na tatizo la kuvuka kwenye mto
wenye maji mengi jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao.
Post a Comment