Ads (728x90)

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla(mwenye miwani) akipata maelezo kuhusu shamba la mifugo la chuo cha Utafiti cha Uyole kutoka kwa Meneja wa mradi huo Dkt Fumbuka Mwakilembe(mwenye shati la kitenge) kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyerembe Munassa

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na watafiti wa kituo cha Utafiti wa Kilimo na Mifugo Uyole
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiwa katika kundi la Ng'ombe wanaofugwa kwenye shamba la Mifugo la la kituo cha Utafiti Uyole
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametoa somo kwa taasisi za utafiti wa kilimo, mifugo wa chuo cha kilimo Uyole akiwataka kuwekeza zaidi kwenye  utafiti ili kutoa wataalaam bora wa kilimo na ufugaji.
Makalla amesema ili kujitosheleza kwa chakula na mazao ya mifugo nchini wataalamu bora wa utafiti wanahitajika ikiwa ni pamoja na kuwa na malighafi ya Viwanda.
Amesema Rais Dkt John Pombe Magufuli anataka nchi iwe na viwanda vidogo, viwanda vya Kati na vikubwa na kwamba viwanda hivyo vitategemea zaidi malighafi za ndani ambazo zitatokana na kilimo cha kitaalamu sanjari na upatikanaji wa pembejeo bora za kilimo.
Amefafanua kuwa nchi yoyote inayowekeza kwenye utafiti huondokana na matatizo ya kukosekana kwa mbegu bora za mazao ya kilimo na mifugo na hivyo jambo pekee la taasisi za Uyole kutumia teknolojia ya kisasa kwa usindikaji wa mazao ili kuyaongezea thamani.
 Kadhalika Makalla amewataka maofisa kilimo,vikundi vya wakulima na wafugaji kutembelea chuo cha Utafiti Uyole ili kujifunza mambo mbalimbali ya kilimo na ufugaji ili kuzalisha kwa tija.

Post a Comment