James Mwampondele (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanahabari baada ya kuchaguliwa kuwa Katibu Uchumi na Fedha wa CCM mkoa wa Mbeya. |
Mwandishi wa habari na mwkilishi wa gazeti la Chama (UHURU) mkoa wa Mbeya Solomon Mwansele akimpongeza kwa kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Uchumi na Fedha mkoa wa Mbeya James Mwampondele |
MJASIRIAMALI
na mwekezaji Jijini Mbeya James Mwampondele(50) ameshinda nafasi ya Katibu Uchumi
na Fedha ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoani Mbeya kwa kupata jumla ya kura 36
kati ya kura 65 za wajumbe wote wa uchaguzi huo.
Mwampondele
aliwabwaga wapinzani wake aliochuana nao vikali katika uchaguzi huo ambao ni Steven Mwakajumilo aliyepata kura 25 na Mshereheshaji mashuhuri Jijini Mbeya
Charles Mwakipesile aliyepata kura 4.
Wagombea
Mwakajumilo na Mwakipesile waliwahi kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi
mkuu kuwania nafasi ya Ubunge na kushindwa kwenye mchujo wa ndani wa CCM ambapo
Mwakipesile aliwania Jimbo la Mbeya mjini na Mwakajumilo aliwania jimbo la
Busokelo.
Nafasi hiyo
iliachwa wazi baada ya aliyekuwa Katibu
Uchumi na Fedha wa mkoa wa Mbeya Hans Mwakisyala kufariki dunia kabla ya
kumaliza muda wake uliotarajiwa kumalizika Julai mwaka huu.
Mwakisyala
alipokea kijiti kutoka kwa Kenneth Ndingo aliyedumu katika nafasi hiyo kwa
jumla ya miaka 15 hadi mwaka 2014 alipoamua kupumzika.
Akizungumza mara
baada ya kuchaguliwa nafasi hiyo Mwampondele aliwashukuru wanachama wa CCM kwa
kumuunga mkono na kuahidi kuendeleza mazuri ya mtangulizi wake ambapo pia aliomba ushirikiano wa hali na
mali kwa viongozi wa chama.
‘’Kwanza namshukuru
Mwenyezi Mungu, pili nawashukuru wana CCM wote pamoja na viongozi wangu bila
kuwasahau wagombea wenzangu, naahidi kushirikiana nanyi kwa hali na mali katika
kusimamia sera na ilani za chama chetu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi,’’alisema
Mwampondele.
Post a Comment