Watumishi na watendaji wa Halmashauri ya Wanging'ombe wakiwa pamoja na wawezeshaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anatory Choya. |
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anatory Choya akizindua mradi wa Uimarishaji Mfumo wa Sekta za Umma unaofadhiliwa na USAID/TANZANIA |
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anatory Choya akiteta jambo na Kiongozi wa timu ya uzinduzi Dkt Peter Kilima nje ya ukumbi wa Kyando mkoani Njombe |
Kiongozi wa timu ya Uzinduzi Dkt Peter Kilima akitoa taarifa za uzinduzi wa mradi Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma. |
Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Rasilimali watu Ofisi ya Rais TAMISEMI Miriam Mmbaga akifafanua jambo wakati wa Uzinduzi wa mradi wa Uimarishaji wa mifumo ya Sekta za Umma. |
Ukumbi wa Mikutano wa Kyando mjini Njombe |
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anatory Choya akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Makete Daudi Yassin wakati wa uzinduzi wa uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma |
SHIRIKA la
msaada la Marekani USAID limekuja na muarobaini utakaoweza kuzisaidia
Halmashauri za miji, Manispaa na Majiji kuepukana na hati chafu kwa kuanzisha
mradi wa Uimarishaji wa mifumo ya Sekta za Umma PS3.
Mradi huo wa
wenye gharama ya Dola milioni 62 utaanza kutekelezwa kwenye halmashauri 93 za miko 13 ya Njombe,Iringa,Morogoro,Mbeya,Lindi,Mtwara,
Rukwa, Dodoma,Kigoma,Kagera, Mwanza,Shinyanga na Mara.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mradi huo mkoani Njombe Kiongozi wa timu ya Uzinduzi wa
mradi huo Dkt. Peter Kilima alisema kuwa mradi huo utazisaidia Halmashauri kujenga
dhana shirikishi katika uimarisha mifumo ya sekta za utendaji kwa umma.
Alisema
mradi huo wa miaka mitano umeanza Julai 2015 ambao utaendelea hadi Julai 2020
ambapo matarajio kila halmashauri katika halmashauri 93 zitafikiwa na mradi
huo.
Dkt. Kilima
alisema mifumo ya utekelezaji ipo katika sehemu 5 za Rasilimali watu,Rasilimali
fedha,Mfumo wa TEHAMA na Tafiti Tendaji ambapo kwa sasa imeshazinduliwa katika
mikoa 7 ya Iringa,Shinyanga,Dodoma,Mwanza,Mbeya, Mtwara na Rukwa.
Alisema
mradi huo umbao umeandaliwa kwa kushirikiana na serikali ya Marekani na
Tanzania unatekelezwa na mashirika saba yakiwemo ya Kitaifa na Kimataifa ambayo
ni Abt Associates Inc ambaye ndiye mtekelezaji mkuu pamoja na watekelezaji
wasaidizi.
‘’Mradi huo
utaimarisha mfumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri, utahakikisha
mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua
zilizoundwa’’alisema.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Rasilimali watu,Ofisi ya Rais TAMISEMI,
Miriam Mmbaga alisema mradi huu utatoa msaada wa kitaaluma katika ,kuimarisha
mifumo iliyopo kwenye utawala wenye lengo la ushirikishwaji katika kuboresha
utoaji huduma kwa jamii.
‘’Zipo
changamoto zinazofahamika kwa watendaji,ushirikishwaji kwa watumishi wa
halmashauri utasaidia kuboresha mahusiano’’alisema Mmbaga.
Awali Kaimu
Mkuu wa mkoa wa Njombe Anatory Choya alisema wadau wa Halmashauri za wilaya
wanapaswa kutumia vyema fursa hiyo kwa kuwa mradi huo ni muhimu kwa maendeleo
ya mkoa na wilaya kwa ujumla.
Uzinduzi wa
mradi huo umefanyika mkoani Njombe kwa kuwahusisha wakuu wa wilaya,
wakurugenzi,wenyeviti wa halmashauri na wakuu wa idara wapatao 170 wa mkoa huo.
Post a Comment