Ads (728x90)

Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya sabini, kuna wimbo mmoja maarufu nilikuwa naupenda sana kuuimba, ulikuwa ukiitwa ''Dont Stop Till U get Enough.....Kibo Kibo Master, wakati ule nilikuwa nashindwa kusema vizuri maneno haya nikawa na nasema Donstopu ligerino, Kibo Kibo Master!!!, alikuwa ni Michael Jackson wakati ule akiwa na kundi zima la Jackson 5 pamoja na kaka zake Jemaine, Tito, Latoya, Marlon na yeye Michael Jackson.

Wakati huo huyu dada yake Jannet Jackson alikuwa bado kinda katika ulimwengu huu wa muziki.

Michael ambaye kwa sasa ni marehemu alijizolea sifa lukuki hususani katika kuwa muasisi wa muziki wa pop ambapo wanamuziki wengi duniani wakiwemo wanamuziki wa kizazi kipya wameiga mtindo wa uchezaji wa 'The Wacko'.

Uchezaji huu wa The Wacko Jacko uliigwa hata na wachezaji wa disco katika ule mtindo maarufu wa 'Break Dance' kabla ya kuzuka kwa mtindo mwingine wa ROBOT ambao vijana wengi wa muziki wa disco wakati ule watakumbuka katika kumbi mbalimbali za starehe kote nchini.

Ni huyu mwanamuziki mahiri muasisi wa muziki wa Pop ambaye amejizolea umaarufu na utajiri mkubwa kutokana na fani yake MICHAEL JACKSON hatunaye tena duniani.

Aliweza kufanya mnegi ikiwemo kuchangia wasio jiweza kama alivyoshiriki na wanamuziki wenzie katika wimbo ule wa We are The Word We are The Children.

Post a Comment