Ads (728x90)

Wakati wa utawala wa Zanzibar ilikuwa makao ya liwali ya Sultani kwa ajili ya pwani la kusini la Tanganyika ikichukua nafasi ya Kilwa Kisiwani kama mji muhimu katika sehemu hii ya pwani la kusini.
Ilikuwa makao makuu ya wilaya tangu zamani ya ukoloni wa Kijerumani. Wakati wa vita ya Abushiri iliona mapigano dhidi ya Wajerumani na wawakilishi wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki waliuawa tar. 22 Septemba 1888. Mei 1890 Wajerumani walirudi chini ya meja Hermann von Wissmann wakateka mji bila upinzani.
Wakati wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani Kilwa Kivinje ilikuwa makao makuu ya mkoa wa nane iliyoenea kati ya Rufiji na Lindi. Utawala wa Kijerumani kilikwisha tar. 7 Septemba 1916 siku ambako Wajerumani waliobaki mjini walijisalimisha mbele ya kikosi cha wanamaji Waingereza.
Mji uliendelea kuwa makao makuu ya wilaya chini ya Waingereza.
Wilaya hii ina sehemu za kihistoria ambazo ni hasa
Kilwa Kisiwani - ambayo ni mfano bora wa miji ya Waswahili wa kale uliojulikana kimataifa tangu karne ya 13 BK
Kilwa Kivinje - iliyokuwa makao makuu ya eneo chini ya masultani wa Zanzibar na wakati wa ukoloni
Songo Mnara - maghofu ya mji wa Waswahili wa kale

Tangu kuondoka kwa makao makuu ya wilaya mji umerudi nyuma. Nyumba za ghorofa za wafanyabiashara hazitumiki tena zimeanza kuporomoka. Boma la Kale la Wajerumani bado inatumika.
Hospitali ya wilaya imebaki Kilwa Kivinje. Tarafa ina wakazi 13,374 (2002). Bandari ndogo inafaa jahazi tu.CHANZO www.wikipedia.org

Post a Comment