Ads (728x90)

Mambo vipi washikaji, mngali mpo katika vitundu vyenu ama mmeamka kutafakari ya dunia, yale yawatafunayo na yale muyatafunayo, mkitafuna jueni iko siku yatawatafuna, kuleni kwa wasaaa, bali msilewe mkila mkakosa mustakabali hata wa kuziongoza kumudu utashi katika familia zenu seuze kuwa na mamlaka ya kuongoza jamii ya watu wanaokaribia milioni 40.

Ni hatari lakini ni salama kila siku ni usanii na sanaa ambazo hazina matokeo mujarabu kwa walala hoi na wale walala hai, hayo ndiyo maisha ya kila siku watu wanaotarajia maisha bora, huku wengine wakila na kusaza tena hula bila hata kunawa mikono, ni aibu tupu, ni nani atakaye ibuikua kuokoa jamii hii ya Wadanganyika huku kila siku zinabuniwa mbinu mbadala za wizi wa kula na kura.

Ni aibu hii kwa wadanganyika waliojifunika blanketi gubigubi na kujivika miwani ya mbao Mintaarafu wasione kilicho mbele yao, na kusahau kilichojiri kabla ya kufikia siku waliyonayo hivi sasa, ni usanii na ni hatari kutumika ili kuwanufaisha wachache wanaoamua kujishibisha matumbo yao, hawaoni hata dhambi kwa Mwenyezi Mungu kufanya mambo haya ya aibu LOOOO!!!!! , Mungu ona udhalili huu na ikiwezekana toa adhabu inayostahili kulingana na matendo yao hapa hapa duniani.

Wakatabahu

Post a Comment