Ads (728x90)

Juni 16, kila mwaka ni siku ya kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika, ikiwa ni kumbukumbu kwa watoto waliouawa kikatili huku katika kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya kusini enzi zile za utawala wa kimabavu na kibaguzi, kufuatia hali hiyo,ikaanzishwa siku maalumu kwa ajili ya kuwakumbuka watoto hao.

Sanjari na kuadhimisha siku hii ya mtoto wa Afrika,watoto wanahitaji kupewa malezi bora, kupewa elimu, kuthaminiwa utu wao ikiwa ni njia pekee ya kuwajali na kuepuka unyanyasaji dhidi yao.

Katika kijiji cha Ilundo kitongoji cha Ibaga, kata ya Kiwira wilayani Rungwe kumetokea unyama wa aina yake baada ya watoto wadogo wanaosoma darasa la nne katika shule ya msingi Ibaga kubakwa na Kibabu chenye umri wa miaka 70 na hatimaye kibabu hicho kuendelea kuvinjari katika mitaa kadhaa ya mkoa wa Mbeya bila kuchukuliwa hatua za kisheria.

Nini hatima ya hili jambo?, ni lini unyanyasaji wa aina hii utakomeshwa?, ni nani mwenye mamlaka ya kulinda haki za watoto hawa, mzazi, mlezi ama kila mmoja wetu, muhimu hapa ni kubadilika kimaadili na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya watu wanaodiriki kuvaa roho ya zaidi ya unyama, kwani hata hao wanyama kwa wanyama hawathubutu kuwadharau wanyama wenzao.

Wakatabahu.

Post a Comment