Ads (728x90)

Mama huyu mfanyabioashara wa nyanya katika moja ya miji hapa nchini akijikimu kwa kuuza nyanya na vitunguu katika mazingira ambayo kwa macho tu ya mtazamaji yanatia kichefuchefu, lakini kwa mujibu wa mama huyu ni kwamba eneo hili la biashara lina baraka za Halmashauri ya mji husika na wapo watoza ushuru maalumu ambao wanawajibika kutoa takataka eneo hilo.
 Umati wa wananchi hukusanyika hapo kwa ajili ya kununua bidhaa katika mazingira hayo bila kujali athari za kiafya.
 Mama huyu ni mtoza ushuru wa eneo hilo, hakuna anachoweza kueleza juu ya mrundikano wa uchafu katika soko hilo linalofanya kazi kila mwisho wa wiki ahata hiyo fursa ya kuweka maandalizi ya usafi siku moja kabla ya siku ya usafi nalo linashindikana.
 Hata watoto nao hulazimika kujikita katika biashara katika mazingira haya ambao hujikusanyia senti kwa ajili ya matumizi ya shuleni.
 Kila kona ya eneo hilo ni uchafu mtupu....jamaa hawaaoni hata aibu kwamba wananchi hawa wanasaidia katika kuongeza kipato ndani ya Halmashauri yao.
Bidhaa za matunda kama vile Maparachichi na nyinginezo ambazo ni marafiki wa INZI pia zipo katika soko hilo ambalo limezungukwa na uchafu kila kona......TAHADHARI  CHUKUA HATUA!!!!!

Post a Comment