NYUMBA 100
zimejengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)mkoani Arusha ili kukidhi
mahitaji ya ongezeko la wakazi na kukua kwa kasi kwa Jiji hilo la kitalii lililopo
mpakani mwa Tanzania na nchi jirani ya Kenya.
Idadi hiyo
ya nyumba ni kati ya nyumba za makazi 98 zilizopo katika eneo la Levolosi na
Meru ikiwa ni mpango wa Taifa wa shirika hilo kujenga jumla ya nyumba 15,000 kwa
kuanzia mwaka 2010 - 2015.
Akizungumza
juu ya mkakati wa shirika hilo kuborsha makazi ya wakazi wa jiji hilo Meneja wa
mkoa wa NHC mkoa wa Arusha Bw. James Kisarika alisema kuwa asilimia 30 ya
nyumba hizo zitapangishwa na nyingine zitauzwa kwa wananchi kulingana na
mahitaji na hali zao za kiuchumi.
‘’Nyumba
zetu zimejengwa na kuuzwa kwa madaraja ya watu wa zote,watu wa hali ya kawaida,
wa kati na wa hali ya juu,’’alisema Bw. Kisarika.
Alisema kuwa hadi sasa Shirika limebakisha jumla
ya nyumba 38 ambazo baadhi yake zitapangishwa na nyingine zitaendelea kuuzwa kulingana
na mahitaji ya wanunuzi.
Bw. Kisarika
alisema kuwa shirika litaendelea kuboresha nyumba zake kwa kuzibomoa na kujenga
upya ambapo wapangaji waliopo katika nyumba hizo watahamishiwa katika nyumba
mpya za shirika.
Kwa upande
wake Ofisa mauzo na masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoani humo Bw.Gibson
Mwaigomole alisema kuwa shirika limeamua kuboresha makazi ya Jiji la Arusha kwa
kuongeza majiji mengine mawili ambayo yatakuwa na nyumba bora za kisasa.
Alisema kuwa
shirika limetenga jumla ya hekari 900 katika maeneo mawili ya USA River lililopo
km 18 kutoka katikati ya Jiji lenye hekari 600 na Safari lililopo eneo la Matevesi
km 10 kutoka katikati ya jiji lenye
jumla ya hekari 300 na kwamba mara mradi utakapoanza nyumba mpya za kisasa zitaanza
kujengwa.
|
Post a Comment