Ads (728x90)

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIMKABIDHI ZAWADI YA UFANYAKAZI BORA MENEJA WA SHIRIKA LA NYUMBA MKOANI ARUSHA BW. JAMES KISARIKA KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI YALIYOFANYIKA KITAIFA MKOANI MBEYA

KILA MWANANCHI ALAIYEINGIA KATIKA UWANJA WA KUMBUKUMBU YA SOKOINE KWA AJILI YA KUSHUHUDIA SHEREHE ZA MEI MOSI ALILAZIMIKA KUPEKULIWA  MLANGONI KAMA UNAVYOONA PICHANI WANANCHI WAKIKAGULIWA KABLA YA KUINGIA KWA MTAMBO MAALUMU

UKAGUZI UNAENDELEA MLANGONI, WANANCHI WATAHAYARI KUONA HALI HIYO YA ULINZI ILIVYOIMARISHA TOFAUTI NA WAKATI MWINGINE


WABUNGE WA MKOA WA MBEYA NAO WALIHUDHURIA SHEREHE HIZO, MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI MAARUFU KWA JINA LA SUGU AKIWA NA WABUNGE WENZI WA VITI MAALUMU, NYUMA YAKE YUPO MARY MWANJELWA NA NAOMI KAIHULA

WANAHABARI KAMA KAWAIDA YAO WALITAMBULIKA KWA VITAMBULISHO MAALUMU VILIVYOTOLEWA ILI KURAHISISHA KAZI WAKATI WA KUCHUKUA MATUKIO UWANJANI HAPO

GARI LA POLISI LIKIWA LIMEONGOZA ,MSAFARA WA RAISI LIKIWASILI KATIKA IUWANJA WA SOKOINE KWA AJILI YA MAADHIMISHO YA MEI MOSI

WANAHABARI WA VYOMBO MBALIMBALI WALIKAA SEHEMU MAALUMU KWA AJILI YA KUCHUKUA MATUKIO YA SHEREHE ZA MEI MOSI

MPIGA PICHA WA RAIS, FREDY MARO ALIKUWA NI MWANAHABARI PEKEE ALIYEKUWA NA FURSA KWENDA HUKU NA KULE KWA AJILI YA KUPATA MATUKIO MBALIMBALI BILA KUZUIWA NA WANAUSALAMA

BAADHI YA WANAHABARI WALIJIKUTA WAKITAFAKARI "KIBUNGE"NADHANI HII ILIKUWA IMETOKANA NA UCHOVU WA SAFARI AMA VINGINEVYO

WAPIGA PICHA WA TELEVISHENI YA TAIFA TBC WALIKUWA KATIKA HARAKATI ZA KURUSHA MATANGAZO HAYO 'LIVE' KUPITIA MAMILIONI YA WANANCHGI WALIOKO NJE YA MKOA WA MBEYA NA WALE WALIOKO MAJUMBANI


MENEJA MKUU WA     SHIRIKA LA NYUMBA MKOA WA ARUSHA JAMES KISARIKA AKIPOKEA KITITA CHA FEDHA IKIWA NI ZAWADI YA UTUMISHI BORA

ILIKUWA NI FURSA NYINGINE YA UZINDUZI WA GAZETI KONGWE LA CHAMA CHA WAFANYAKAZI NCHINI MAARUFU KWA JINA LA MFANYAKAZI AMBALO LIMEREJEA TENA

RAIS KIKWETE PIA ALICHUKUA FURSA NYINGINE YA KUMKABIDHI ZAWADI MKURUGENZI WA JIJI LA MBEYA AMBAYE NAYE ALIJIZOLEA KITITA CHA FEDHA TASLIMU


KAMA ILIVYO KAWAIDA KATIKA MAONESHO VITUKO HAVIKOSEKANI KAMA INAVYOONEKANA PICHANI, GARI HILI LA AINA YAKE LILIPITA KATIKA MAANDAMANO LIKIWA NA UJUMBE ULIOULIZA; KWANINI TUWE MASKINI NA NCHI YETU TAJIRI



Post a Comment