WATU watano wenye
silaha wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambao hawajatambulika majina yao wameuawa
jana mchana katika kijiji CHA Galijembe nje kidogo ya Jiji la Mbeya baada mapambano
ya kurushiana risasi kati yao na askari polisi wa mkoa huo.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari jana jioni kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Bw.
Diwani Athumani amesema kuwa watu hao ambao walikutwa na bunduki mbili aina ya
SMG yenye risasi 16 na MARK III yenye risasi
mbili katika magazine.
Kamanda
Diwani amesema kuwa watu hao waliokuwa katika gari yenye namba za usajili T 911
BUG aina ya Toyota Spacio walikuwa na dalili za kufanya mauaji na uhalifu mkubwa
katika maeneo ya Tukuyu,Ushirika na Uyole.
Amesema kuwa
kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia Jeshi la Polisi lilifuatilia neyndo za
watu hao katika maeneo mbalimbali ili kuzuia tukio lolote la mauaji na uhalifu
ambao ungeweza kutokea katika siku mbili hizi.
Kamanda
Diwani amesema kuwa wakiwa katika doria ya kawaida walilisimamisha gari
lililokuwa na washukiwa hao wa ujambazi ambapo lilisimama vizuri na baadaye
ghafla watu wawili walitoka nje ya gari na kurusha ovyo risasi wakielekeza eneo
ambalo walikuwepo askari polisi.
Amesema hata
hivyo risasi zao hazikuweza kuwakuta askari polisi bali watu hao watano
walijeruhiwa kwa risasi katika maeneo mbalimbali ya miili yao na baadaye
kufariki dunia wakiwa katika hospitali ya rufaa ya Jijini Mbeya.
Amesema kuwa
mbali na bunduki mbili walizokutwa nazo walikuwa na kamba maalumu ambayo
inatumiwa kwa namna mbalimbali za uhalifu ikiwemo kuwafunga watu waliotekwa na
baadhi ya mizigo watakayoiba na kwamba kamba hiyo haikatiki kwa urahisi.
|
Post a Comment