|  | 
| Wananchi walijitokeza kwa wingi katika maandamano ya kilele cha siku ya Red Cross yaliyofanyika Kitaifa Jijini Mbeya, waendesha Boda boda walishiriki mandamano. | 
|  | 
| Maandamano hayo yaliyoanzisha Mafiat na kupita barabara kuu ya Dar-Zambia kiasi cha mwendo wa km 2 yaliongozwa na Brass Band ya Magereza ya Mkoani Mbeya. | 
|  | 
| Vijana wa Skauti walishiriki maandamano hayo. | 
|  | 
| Mamia ya wakazi wa Jiji la Mbeya walishiriki maandamano hayo ya kilele cha maadhimisho ya siku ya Msalama Mwekundu Duniani ambayo Kitaifa yalifanyika Mkoani Mbeya. | 
|  | 
| Baadhi ya waandishi wa habari walishiriki katika kupata taarifa za maadhimisho hayo | 
|  | 
| Makamu wa Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Dkt. Zainab Gama akisoma risala maalum ya chama cha Msalaba mwekundu nchini | 
|  | 
| Mwandishi wa Habari Mwakilishi wa TBC mkoani Mbeya Hosea Cheyo akiwa na cheti cha Heshima cha kuthaminini ushiriki wa chombo hicho kwenye maadhimisho hayo. | 
|  | 
| Emmanuel Lengwa mwakilishi wa ITV/Redio One na Hosea Cheyo Mwakilishi wa TBC wakiwa na vyeti vya heshima siku ya Red Cross mkoani Mbeya. | 
|  | 
| Wanahabari wakibadilishana mawazo wakati wa kilele cha maadhimisho hayo. | 
|  | 
| Nderemo na Vifijo viliendelea hadi saa mbili usiku wakati wa ugawaji wa zawadi kwa timu za mpira wa miguu zilizoshiriki katika michezo kwenye wiki ya Msalaba Mwekundu. | 
|  | 
| Wananchi wakijimwaga mwaga kwenye maadhimisho ya kilele cha sherehe za Msalaba mwekundu mkoani Mbeya | 
















Post a Comment