MKUU wa Mkoa
wa Katavi Dkt.Rajabu Rutengwe ameshauri teknolojia ya habari na Mawasiliano
ifike vijijini ili iwawezeshe wakulima kwenda na wakati katika kutathmini
bidhaa zao za kilimo.
Dkt.Rutengwe
alisema hayo wakati wa majumuisho ya kwenye maonesho ya Kilimo Nane Nane katika
ukumbi wa Banda la Mifugo leo mchana.
Alisema bidhaa
zinazooneshwa na wakulima zikitangazwa zitajulikana kimataifa nakuwa ni muhimu kwa kila Halmashauri kujianzishia
tovuti na Blogu ili ziendane na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.
Dkt.Rutengwe
alisema kuwa kilimo cha kisasa kinapaswa
kwenda na wakati uliopo ambao wananchi wanahitaji kupata taarifa za bei za
mazao na masoko kutoka maeneo mbalimbali nchini.
‘’Halmashauri
zitangaze mambo yao katika mitandao ya kijamii, magazeti na Runinga ili taarifa
zao za utendaji zifahamike vyema kwa wananchi’’, alisema.
Aidha Dkt.Rutengwe aliwataka wakulima kutumia
pembejeo na kuachana na dhana ya ardhi kutokubali mbolea na kuwa dhana hizo ni
potofu ambazo zinasababisha wakulima kuzalisha chini ya matarajio ya kila
mwaka.
‘’Tungeweza
kufanya vizuri tungetumia mbolea na mbegu bora,ni muhimu mabadiliko ya kilimo
yaendane na kasi ya kilimo bora kinachotokana na uzalishaji wenye tija,’’alisema.
|
Post a Comment