TAKRIBANI Abiria 40 waliokuwa wakisafiri kwa basi la kampuni ya Majinja aina ya SCANIA lenye namba za usajili T 438 CDE linalofanya safari zake kutokea Mbeya kuelekea Jijini Dar es salaam wahofiwa kufa baada ya basi hilo kugongana na Lori lililobeba Kontena ambalo lilikuwa linafanya safari zake kutokea Dar es salaam kuelekea Jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba ajali hiyo
imetokea majira ya saa 4:30 asubuhi eneo la Changarawe mjini Mafinga ambapo
dereva wa Basi alikuwa akikwepa mashimo kwenye barabara hiyo ilhali dereva wa
Lori naye alikuwa alikuwa akikwepa mashimo na baadaye magari hayo kugongana uso
kwa uso.
Imeelezwa kuwa mara baada ya magari hayo kugongana Lori
ambalo lilikuwa na Kontena lilipanda juu ya Basi na kuliminya na kusababisha
vifo vya abiria waliokuwemo kwenye basi hilo.
Shuhuda wa tukio hilo alisema kuwa ni abiria watatu akiwemo
mtoto mmoja ndio wanaodaiwa kunusurika katika ajali hiyo na kwamba miili ya
marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Mufindi iliyopo Mafinga
ambapo zoezi la kuzitambua maiti linaendelea muda huu.
Post a Comment