Mtoto mwenye ulemavu wa ngiozi Baraka Cosmas(6) akiwa wodi namba nane Hopaitali ya Rufaa Mbeya ambako amelazwa kutokana na jeraha la kukatwa kiganja chake cha mkono kwa imani za ushirikina. |
Wakuu wa mikoa Stellah Manyanya(Rukwa) Abbas Kandoro(Mbeya) wakiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya kumjulia hali mtoto alkiyekatwa kiganja chake cha mkono kwa imani za kishirikina. |
NI majira ya
mchana saa 7: 30 katika hospitali ya Rufaa Mbeya!! ambako amelazwa mtoto mwenye
ulemavu wa ngozi(ALBINO) aliyejeruhiwa kwa kukatwa mkono wake wa kuume na mtu asiyejulikana huko katika
kijiji cha Kipeta wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.
Wakuu wa
mikoa Abbas Kandoro (Mbeya)na Stellah Manyanya(Rukwa) wakiongozana kumtembelea
mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Baraka Cosmas(6) ambaye amekatwa kiganja chake
cha mkono wa kuume na watu wasiojulikana kisha kuondoka nacho.
Simanzi na
majonzi vilitawala katika wodi namba 8 ya Hospitali hiyo yenye sifa ya
kuhudumia mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambapo wagonjwa na wananchi wengine
walijikuta wakibubujikwa na machozi walipomshuhudia mtoto huyu asiye na hatia
akiwa na mkono usio na kiganja.
Mama wa
mtoto huyu Prisca Shaaban(27) ambaye pia alijeruhiwa kwa kupigwa na kitu kwa
kupigwa na rungu kichwani anaeleza mkasa uliomsibu siku ya uvamizi.
‘’Ulikuwa
usiku wa manane, mtu aliingia ndani na kunitaka nimpe mtoto aende naye,
nilikataa akanipiga na rungu kichwani nikapoteza fahamu,akamkata mtoto kiganja
cha mkono wa kulia na kuondoka nacho’’
Ama kwa
hakika ni unyama wa hali ya juu ambao haukustahili kufanyiwa binadamu kwa
binadamu mwenzie, katika mazingira ya kawaida ni vigumu kuamini aina hii ya
ushirikina kama ina tija kwa wanaofanya ushirikina huu, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Stellah Manyanya ana haya ya kusema;
‘’Si kweli
kama viungo vya Albino ni mali, kwani ingekuwa hivyo hata hao alibino wenyewe
wangeanza kuwa matajiri kutokana na hali yao, haya ni mambo ya kishetani ambayo
msingi wake sijui unatokana na mazingira gani, serikali itaendelea kupiga vita
unyama huu,’’
Naye Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa mikoa yote nchini alisema kuwa
mazingira ya Albino yameendelea kuwa katika hatari kutokana na kukosekana kwa
ushirikiano baina ya wananchi kwa kuwa ‘’ wauaji wa albino wapo kati yetu
tunaishi na kula nao,’’.
Kiongozi wa
wenye ulemavu Claud Mwakyoma alisema kuwa kama serikali ina uwezo wa kuwalinda
tembo wasiuawe na majangiri wanashindwaje kuwalindaa binadamu wenzao na kwamba
inawezekana ulinzi dhidi ya Albino ni mgumu sana hivyo ni vyema basi
wakapelekwa gerezani ili waishi kama wafungwa.
‘’Naamini
tukienda kuishi magereza huko kuna ulinzi wa kutosha kwa kuwa huku nje hatuna ulinzi
na tunaendelea kuangamizwa kwa kuchinjwa na kuuawa,’’alisema Mwakyoma.
Prisca ana
jumla ya watoto wanne watatu kati yao ni walemavu wa ngozi ambapo mmoja wao ni
huyu aliyekatwa mkono, ameiomba serikali imsaidie kumlinda kutokana na hofu ya
maisha aliyonayo.
‘’Nina
watoto wanne Baraka(6) aliyekatwa mkono,Lucia(3) na Shukuru(9) ambapo mtoto
pekee ambaye asiye na ulemavu ni Jafar(11)’’ alisema.
Alibainisha
kuwa siku ya tukio hilo mumewe Cosmas Lusambo alikuwa ameenda kulala kwa mke
mdogo ndipo usiku wa manane alipovamiwa na mtu ambaye alitaka kumnyang’anya
mtoto ambaye baadaye alipokataa ndipo alipompiga rungu la kichwani na kumchukua
mtoto na kumkata kiganja cha mkono wa kulia.
Post a Comment