Bado nipo ningalipo,nijapo ndaja kwa tapo,
Naandaa yaliyopo,yaje barizi tulipo,
Tutambe yaso matapo, tuyaunde yaliyopo,
Fasihi njema zi papo, umma blogu usihofu.
Recent Posts
- Rashid Mkwinda03 Sep 2017NaViNjArI TaNzANiA- NILIPOTEMBELEA RAFIKI ZANGU WA KIMAASAI
Nipo na rafiki zangu jamii yaWamaasai tukibadilishana mawazo Nimetembelea rafiki zan...
- Rashid Mkwinda16 Aug 2017SOKO LA SIDO JIJINI MBEYA LILIVYOTEKETEA KWA MOTO JANA USIKU
Eneo la Soko la SIDO jijini Mbeya lilivyokuwa likiteketea kwa moto jana usiku Sok...
- Rashid Mkwinda19 Jul 2017MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA MKE WA DKT MWAKYEMBE KYELA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mke wa Dkt Ha...
- Rashid Mkwinda18 Jul 2017MWILI WA MRS MWAKYEMBE WAWASILI MBEYA JIONI HII, MSAFARA KUELEKEA KYELA
Viongozi wa serikali wa mikoa ya Mbeya na Songwe mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla na Mkuu wa mk...
- Rashid Mkwinda16 Jul 2017RAIS DKT MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KIFO CHA MKE WA DKT. MWAKYEMBE
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...
- Rashid Mkwinda30 Jan 2017GOLIKIPA DAVID BURHANI AFARIKI DUNIA
Aliyewahi kuwa Golikipa wa kutegemewa wa timu za Majimaji ya Songea,Prison na Mbeya Ci...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Nasi twakutazamia
ReplyDeleteUje fikira jazia
Lakini ukitulia
Viboko takuchapia
Tena wazi tamkia
Nyumba ndogo kimbilia
Lini utajarudia
Nyumba kubwa kutunzia?
Tumechoka kusikia
Wanao kutwa lilia
Chakula wakikosea
Babayo mbali lowea!
Kweli uloyasemea, Makene nimesikia,
ReplyDeleteFikira nitajazia,Blogu tafurahia,
Nyumba ndogo sina nia, Blog taimarishia,
Mswada naandalia, Fasihi ilo tulia,
Wana waje furahia, kaburi nikiingia,
Wasome na kujivunia, ya blogu kutokea.
Nangoja huo muswada, ewe mwandishi mvivu
ReplyDeleteVipi njaa ulie shinda,tupa kunako uvungu
Nona washindwa kesha, kalamu yawa machungu
Mkwinda ninakwachia, Riwayani kimbilia.
Kumradhi, maoni yangu hayakujipanga nilivyotaka:
ReplyDeletenangoja huo muswada, ewe mwandishi mvivu
vipi ulie njaa shinda, kipaji tupa kunako uvungu?
Mbona washindwa kesha,kalamu geuza machungu
Mkwinda ninakwachia, Riwayani kimbilia.
Kumradhi, maoni yangu hayakujipanga nilivyotaka:
ReplyDeletenangoja huo muswada, ewe mwandishi mvivu
vipi ulie njaa shinda, kipaji tupa kunako uvungu?
Mbona washindwa kesha,kalamu geuza machungu
Mkwinda ninakwachia, Riwayani kimbilia.
Mkwinda,
ReplyDeleteacha uvivu we malenga!
Nafuatilia mapambano haya ya mistari hii ya kishairi.
Nijapo nena kivivivu,wanenao warizevu,
ReplyDeleteNitambe wacheke mbavu, wana watezee ndevu,
Kamwe si vivu na tambo tambo zangu endelevu, watakari wavivu na wajao na zao nguvu.
Makene, Ndesanjo wajuvu wa tambo zino angavu.
Natamati kutotamba nasubiri tambo angavu.
Makene Ndesanjo, nahitaji Changamoto kwa mswada nilkopandisha katika bLogu vipi mbona kimya mmenywea mlidhani natania nilipowaambia kuwa naandaa mswada? haya kazi kwenu tugangamale tutoa kitabu kitokanacho na wanaBlogu
ReplyDelete