Ads (728x90)

DCP Diwani Athumani RPC-MBEYA
Ernest  Mangu-RPC MWANZA
DCP Thobias Andengenye aliyekuwa RPC Arusha
Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Mwema anayetarajia kustaafu mwishoni mwa mwaka huu

Ni takribani miaka 8 sasa inakaribia kumalizika baada ya uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Interpol Said Mwema kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Omar Mahita ambaye alikuwa IGP kwa takribani miaka 10 akiwa amevaa viatu vya marehemu Harun Mahundi.

Tofauti na aliyekuwa mtangulizi wake Said Mwema amejizolea sifa lukuki za utendaji wake katika Jeshi la Polisi na kuibua dhana nyingi ikiwemo Polisi Jamii, Ulinzi Shirikishi na hata Utii wa Sheria Bila Shuruti.

Kwa kutumia weledi wake wa kazi Mwema ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Interpol alikuwa RPC Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya ambaye alirithi mikoba ya aliyekuwa RPC mkoani humo Laurian Sanya.

Kwa kufuata weledi ule ule wa kazi kutoka kwa mtangulizi wake akiwa RPC mkoani Mbeya aliweza kufanikiwa katika wimbi kubwa la majambazi kwa wakati wake na kupunguza kwa kasi kubwa, tatizo la mauaji ya kishirikina na hata ujambazi wa uporaji na utekaji wa magari.

Kutokana na sifa hiyo na mengine mengi Said Mwema alipata tunu adhimu ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Interpol na baadaye kuteuliwa na Rais kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi nchini akirithi mikoba ya Omar Mahita ambaye alielezwa kutofanikiwa vizuri katika nafasi hiyo.

Wakati wa Mahita kulikuwa na wimbi kubwa la mauaji na hata vitendo vya ukatili vilivyoelezwa kufanywa na Jeshi la Polisi hususani wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 hususani katika Visiwa vya Zanzibar, alijipachika jina maarufu la NGUNGULI kwa kile kilichosemwa kukabiliana na nguvu ya chama cha Wananchi CUF wakati ule maarufu kwa jina la NGANGARI.

IGP Mwema alimudu kuwavuta na kuwaaminisha wananchi kuwa Jeshi hilo lipo kwa ajili ya kuwatumikia Raia na si vinginevyo na hivyo kujaribu kufunika maovu ya mtangulizi wake Mahita ambaye aliwafanya raia wengi kulichukia Jeshi hilo.

Hata hivyo weledi wa IGP Said Mwema ambao umempatia sifa lukuki unaelezwa kuwa unakaribia kufikia tamati mwishoni mwa mwaka huu ambapo VICHWA vitatu vinatajwa kuwa vinaweza kurithi nafasi hiyo kutokana na sifa walizonazo na umahiri na weledi wa utendaji wao ndani ya Jeshi la Polisi nchini.

Wanaotajwa sana kulingana na vyanzo mbalimbali na nukuu katika baadhi ya vyombo vya habari ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya DCP Diwani Athumani,cheo ambacho ametunukiwa hivi karibuni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu na DCP Thobias Andengenye ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha.

Kila mmoja kati ya hao ana sifa zake katika utendaji uliotukuka katika Jeshi hilo ambapo kwa kuweka uwiano wa utendaji wao ndani ya Jeshi la Polisi kila mmoja anazo sifa zinazotajwa kusukuma mbele utendaji wa Jeshi la Polisi nchini.

Kwa kuona umuhimu wa wa kumpata kiongozi mahiri aliyetukuka Blogu hii na Bloga wadau wanaopenda kushiriki katika mchakato huu tunaweka fursa ya wananchi kufuatilia kwa makini utendaji wa Makamanda hawa na hatimaye kupiga kura kupitia FB ambazo zitakuwa wazi kwa wasomaji wa mitandao ya Kijamii kuweka mustakabali wa uongozi ndani ya Jeshi la Polisi nchini.

TUNAAMINI KATIKA UTII BILA KUSHURUTISHWA!!!.

Post a Comment