TAZAMA WAPIGA KURA WA MWAKANI HAWA
Haya ndiyo maisha!!! nilitembelea kijiji kimoja kipo hapa hapa nchini katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya , huko huduma ya maji safi na salama kwao ni sawa na ndoto, waheshimiwa wako bungeni wanapigwa na viyoyozi huku kila mmoja akitetea eti nadiriki kurudi tena bungeni kwa kura za wananchi hawa wanaokunywa maji haya, hivi ni haki hii?hebu Mheshimiwa Esterina Kilasi angalia wapiga kura wako hawa, unatarajia kweli kuommba tena kura zao mwakani kwa hali kama hii?, unajua mazingira wanayoishi?mie sitaki kukwambia hicho ni kijiji gani ni mtihani kwako, kwani kama mbunge nadhani unajua maisha wanayoishi na huduma wanayoipata,hebu jaribu kufikiria iwapo wanakosa huduma ya maji huduma ya afya wanayo kweli,kwa taarifa yako ili kupata huduma ya afya hulazimika kutembea umbali upatao kilomita 85 kufika katika kituo cha Afya, ili kufika katika kijiji hicho nililazimika kutumia siku nzima na kuvuka mito na mabonde.habari hii pia unaweza kuikuta kwenye blog, nilichokiona.blogspot.com
Mwaka 2005 nilifika vijiji karibia vyote vya wilaya za Kyela, Chunya, Rungwe na Mbarali. Lakini Mbarali inatisha. Mazingira ni magumu mno.
ReplyDeleteWabunge wetu, pumzikeni kuomba nyongeza za mishahara na marupurupu mengine, isimamieni serikali itukumbuke na kutuendeleza 'wananchi sisi'
Naam!!! hayo ndio maisha ya wapiga kura na hayo ndiyo maji wanayokunywa kama unavyoona pichani, utadhani wako katika sayari nyingine, hao ni Watanzania iliyo huru tangu mwaka 1961
ReplyDelete