Ads (728x90)



Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika... piga nikupige...risasi za moto....mabomu ya machozi....mawe...virungu na hatimaye vijana zaidi ya 88 kutiwa rupango, ni kutokana na mauaji ya mfanyabishara anayedaiwa kuuawa na askari polisi w akituo cha Tunduma kwa madai kuwa alimdhania kuwa ni jambazi.Hiyo ndiyo hukumu yake hata kama alikuwa mtuhumiwa wa ujambazi?, ndiyo sheria ilivyo? nini hasara ya kuchukua sheria mkononi. Alikuwa ni mfanyabiashara mjasiriamali aliyejitafutia riziki yake na kupata mafanikio, ameuawa na askari polisi,..polisi ilishindwa kutumia mbinu za kumtia hatiani, tena basi aliuawa hatua chache akiwa karibu na nyumbani kwake kabla ya kuuawa alifukuzwa kwa mwendo wa kilomita kadhaa na gari lake kupigwa risasi na kusimama....tume imeundwa kuchunguza tukio hili, nini hatima ya utawala wa sheria na utumishi unaozingatia maadili kwa watendaji wa serikali?

Post a Comment