Ads (728x90)



Ilikuwa ni siku ya furaha na faraja kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya wazazi META wakati wa siku ya 'MEDIA DAY', kundi la waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya walijikusanya na kuwatembelea wagonjwa na kutoa msaada wa vyandarua na sabuni kwa akina mama na watoto waliolazwa katika hospitali ya wazazi Meta jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari duniani. Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya akiwemo Mwanafasihi wa safu hii (kulia kabisa mwenye kamera) wakipanda ngazi kuelekea ndani ya ghorofa ya kwanza ambako akina mama wazazi waliojifungua wamelazwa, hii ilikuwa ni mwaka 2007.

Post a Comment

  1. Kaka hatimaye nimetembelea uwanja wako,na ghafla nimevutiwa sana na tukio hili.
    Na pia nimewaona wadau ambao nilibahatika kufanya nao kazi wakati huo.
    kweli maisha ni mzunguko,salamu zangu kwa wadau hao wanaonekana katika picha hii.

    ReplyDelete