KARIBU mkoani Mbeya Bw. Abbas Kandoro unahamia mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuendeleza gurumu la maendeleo ya Taifa letu,naamini hukufikiria kuwa utakuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya,bali kutokana na fikra za aliyekuteua aliamini kuwa ukiwa Mbeya unaweza kufanya lile ambalo linawafaa wakazi wa mkoa huo.Jambo unalopaswa kulijua ni kuwa mkoa huu una mengi ya kuigwa na pia yapo mengi ya kuyapuuza, katika yale yanayofaa kuyapuuza ni pamoja na umbeya na majungu ambayo yamewaangusha wengi walioamua kuyafuatilia na kuacha wajibu wao wa kazi.naamini ukishikilia kamba ya weledi wa kazi,uadilifu na uwajibikaji kamwe hauwezi kuanguka kwa kuwa ipo mifano mingi ya walioendekeza majungu wakaanguka moja kwa moja bila kunyanyuka.
Karibu Mbeya ukiamini kuwa umekuja katika mikoa ambayo viongozi wengi wamepandia hapo ilhali baadhi yao wameangukia pua...Karibu Mzee tuendeleze majukumu ya Kitaifa.
KWAHERI mzee John Mwakipesile...ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa mstaafu, Rais alikuheshimu na kukupa dhamana ya kuuongoza mkoa wa Mbeya kwa takribani miaka sita ambapo kabla ya hapo ulipata kufanya kazi katika mkoa huo ukiwa Mbunge wa jimbo la Kyela na baadaye ulipostaafu Ubunge ukachaguliwa kuwa Mkuu wa mkoa ambapo uliwajibika na kufanya kazi katika mazingira magumu huku ukikabiliana na changamoto lukuki za umbeya na majungu katika mazingira magumu ulifanikiwa kukabiliana nayo na hatimaye kwa kiasi chako ulifanikiwa na leo hii unaachia majukumu hayo kwa Bw.Kandoro.
Kwaheri Mzee Mwakipesile mchango wako tunaauthamini na kamwe hatutausahau weledi wako na uwajibikaji wako utaenziwa na kama binadamu kama kuna mapungufu naamini wengi wamekusamehe kama yapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment