Ads (728x90)

Na,Rashid Mkwinda,Isoka Zambia.

MGOMBEA uchaguzi kwa chama cha Movement for Multpart Democracy (MMD)Bw.Rupia Banda amekubali kushindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo na matokeo yake kutangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi nchini humo kwa mgombea wa Patriotic Front Bw.Michael Sata kuibuka na ushindi.

Tume ya uchaguzi nchini Zambia imemtangaza rasmi Bw.Sata kuwa ni Rais mpya wa Zambia huku nderemo vifijo na vigelegele vikiendelea kuhanikiza katika miji mbalimbali ya nchini Zambia.

Mwandishi wetu aliyefika katika wilaya ya Nakonde,katika miji ya Nakonde na Isoka alishuhudia namna ambavyo wananchi wa maeneo hayo walivyoonesha furaha yao huku wakielezea kuwa ushindi huo ni ushindi wa wananchi wote wa Zambia.
Mkazi wa mjini Isoka aliyejitambulisha kwa jina la Lameck Gondwe alisema kuwa tatizo lililosababisha chama cha MMD kushindwa ni ubadhirifu wa fedha za umma uliokuwa ukifanywa na viongozi wa chama hicho huku wananchi wakikosa huduma bora za afya,elimu na miundo mbinu mibovu.

''Tunatarajia mabadiliko makubwa katika sekta za elimu,afya na miundo mbinu, uongozi wa chama kilichopita hakikujali kabisa maslahi yetu,alisema Bw.Gondwe.

Kwa upande wake Bw.Kabwe Nkonde mkazi wa Nakonde mpakani mwa Zambia na Tanzania alisema kuwa ushindi wa Bw,Sata na chama chake cha PF ni dalili njema kwa Wazambia katika kuelekea kwenye uchumi bora kwa kuwa hivi sasa Kwacha ya Zambia ilikuwa imeporomoka kutoka dola 500 hadi dola 350.

Alisema kuwa wakati wa marehemu rais Levvy Mwanawasa uchumi wa Zambia ulikuwa juu lakini tangu aingine Bw.Banda hali ya uchumi imekuwa ikizidi kuporomoka siku hadi siku na hivyo kusababisha wananchi waishi maisha magumu.

Post a Comment